Mratibu wa mradi Kuhne, Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Omary Swalehe akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusiana na mradi wa masuala ya usafirishaji mijini. mafunzo hayo yamefunguliwa leo Machi 26, 2024 Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.
Kaimu Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Coretha Komba akizungumza wakati wa kufungua mafunzo ya Usafirishaji Mijini kwa wadau wa usafirishaji. Mafunzo hayo yalifanyika Machi 26, 2024 jijini Dar es Salaam.

KATIKA Kuhakikisha Usafiri wa mijini unakuwa wa uhakika na rahisi, Chuo Kikuu Mzumbe kwa Kushirikiana na Taasisi ya  Kuehne Foundation watoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa usafirishaji ili kuhakikisha usafiri huo unakuwa rafiki kwa kila Mwananchi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2024 Mratibu wa Mradi wa huo na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Omary Swalehe, amesema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki kuhusiana na Changamoto za Usafiri mijini pamoja na kupata uvumbuzi wa changamoto katika Usafiri ili uweze kuboreshwa. 

"Lengo la mafunzo ni kuwajengea uwezo washiriki ili kuboresha usafiri mijini, tunajua kabisa usafiri mijini ni Changamoto kubwa katika maana nzima ya msongamano wa magari barabarani, miundombinu pamoja na changamoto zinazoletwa na waendesha pikipiki (Bodaboda) waendesha bajaji na watumiaji wengine ambao hawafuati taratibu."

Amesema mafunzo hayo yatatoa majawabu ya usafirishaji mijini na kutatua changamoto  ya usafiri mijini. 

Akizungumzia namna ambavyo changamoto ya usafiri itakavyo tatuliwa Dkt. Omary amesema kuwa Changamoto za usafiri mijini hazitatuliwa na Serikali peke yake bali ni kushirikisha sekta binafsi pamoja na watumiaji ili kuhakikisha usafiri mijini unakuwa salama, unakuwa wa uhakika na kuwa usafiri wa haraka. 

Dkt. Omary akitolea mfano amesema kuwa Dar es Salaam kunamsongamano wa magari ambapo haijalishi kama upo usafiri wa Umma au binafsi changamoto kuwa ni kutokufika kwa wakati pale ambapo unapoelekea yaani muda mwingi unatumika pamoja na nishati inayotumika kwenye magari inakuwa nyingi na gharama kubwa.

Licha ya hayo Dkt. Omary amesema mafunzo hayo yanatolewa na Chuo Kikuu Mzumbe kupitia mradi wa Kuehne  bila gharama yaani ni bure lakini mwitikio wa wadau wa usafirishaji ni mdogo kwa wakati mwingine. 

Amesema kuwa changamoto wanayokumbana nayo ni kutangaza mafunzo kwa wadau mbalimbali wa usafirishaji ili kutatua changamoto za usafirishaji lakini wanaoomba ni wachache ingawa changamoto ya usafiri ni kubwa.

"Nawaomba  Wadau waweze kuchangamkia fursa hiyo kwani Chuo hiki kinatafuta wadau wenye weredi, wenye utaalamu na uzoefu ili kusaidia watu waliopo kwenye tasnia ya usafirisha na Usafiri ili kujua changamoto na kutafuta namna ya kuzitatu."

"Nina waomba jamii na watanzania wote kuchangamkia fursa pale zinapojitokeza ili kuweza kufikia malengo ya Mradi."

Kwa Upande wa Mwakilishi wa wanaopewa mafunzo hayo amesema kuwa mafunzo hayo yatakwenda kuwasaidia kutafuta njia rahisi ya kurahisisha usafiri mijini bila kutumia muda mwingi pamoja na nishati kubwa bila kuathiri Mazingira.

Katika Mafunzo hayo wapo wahadhiri wa Masuala ya Usafirishaji, Wanavyuo wanaosoma masuala ya Usafirishaji, wengine ni kutoka Halmashauri za wilaya za Mijini pamoja na wadau kutoka taasisi binafsi za masuala ya usafirishaji.

Watoa mada wakitoa maada kwa wadau wa usafirishaji jijini Dar es Salaam leo.


Picha ya Pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...