Na Mwandishi wetu, Simanjiro
MKUU
wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Dkt Suleiman Hassan Serera,
ameendelea na ziara yake ya kutembelea kitongoji kwa kitongoji kwa lengo
la kusikiliza kero na changamoto za jamii.
Dkt
Serera, akizungumza na waandishi wa habari, amesema lengo la ziara yake
ni kuhakikisha wakazi wa vitongoji vyote 278 wanafikiwa na kusikilizwa
ii kutatua matatizo yao.
“Katika
ziara yangu naambatana na wataalamu mbalimbali wakiwemo wa idara ya
afya, elimu, ardhi, maji, barabara na wengineo hivyo watu wakiwa na kero
au changamoto zao wanapatiwa majawabu,” amesema.
Dkt
Serera amesema ataendelea na ziara hiyo kwa kutembelea kitongoji kwa
kitongoji kwa lengo la kuwasikiliza wakazi husika na kuzungumza nao ili
kuendelea kujenga Simanjiro.
Amewapongeza
wakazi wengi wa vitongoji husika kushiriki mikutano hiyo na kuzungumza
kero na changamoto zinazohusu jamii kwa ujumla na siyo matatizo
binafsi.
Diwani wa kata
ya Endiamtu, Lucas Chimba Zacharia, ametoa shukrani kwa Dkt Serera, kwa
kufanya ziara ya kitongoji kwa kitongoji na kusikiliza kero za wakazi
wa eneo hilo.
“Hii ni
mara ya kwanza kwa mkuu wa wilaya kufika ngazi ya kitongoji na kitongoji
na kusikiliza kero za jamii na kuhakikisha zinazoweza kutatuliwa
zinatatuliwa kwa wakati,” amesema.
Diwani
wa kata ya Emboreet, Yohana Shinini amemshukuru mkuu huyo wa Wilaya kwa
kuwatembelea na kuwasikiliza kwani changamoto na kero za vitongoji
zimepata ufumbuzi.
“Hongera
sana mkuu wetu kwa ziara yako kwenye kata ya Emboreet, kitongoji kwa
kitonji, kwani matatizo ya jamii yamepata majawabu na utatuzi wa wa kero
umefanyika,” amesema Shinini.
Mkazi
wa kitongoji cha Kairo, Shiwarael Nyari (Gaakona) mwenye umri wa miaka
70, amemshukuru Dkt Serera kwa namna alivyoweza kuwasaidia kwa kuingilia
kati tozo ya jengo kupitia luku.
“Huwa
tunakatwa fedha ya tozo ya jengo pindi tukilipia ankara ya nishati ya
umeme kwa njia ya luku, tunamshukuru Mhe DC amewasiliana na watu wa
mamlaka ya mapato (TRA) ili tuondolewe hiyo tozo,” amesema Nyari.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...