*Wafurahishwa Na Utekelezaji Wa Miradi Hiyo
WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Stergomena Tax, leo Machi 16, 2024 ameshiriki katika ziara ya Kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya mambo ya Nje,Ulinzi na Usalama kukagua miradi ya maendeleo unayoendeshwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga kupitia Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Maghala ya Kuifadhia VIfaa ya Gongolamboto na Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Kunduchi, Dar-es-salaam.

Kamati hiyo ya Bunge ya Nje,Ulinzi na Usalama iliongozwa na Mwenyekiti wake Mheshimiwa Vita Rashid Mfaume Kawawa ilikagua utekelezaji wa mradi wa maghala mapya yanayojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kambi ya Gongolamboto na baadaye kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi ambapo pia ilikagua mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi za washiriki wa kozi za chuo hicho.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje ,Ulinzi na Usalama iliipongeza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika kusimamia miradi hiyo ya Kimkakati Jeshini na kwa kuhakikisha pesa inayotolewa na Serikali inatimiza malengo yaliyokusudiwa. Aidha Kamati hiyo ya Bunge imeonyesha kufurahishwa Ubora wa majengo na Maghala hayo yanayojengwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...