Misaada mbalimbali imezidi kumiminika kwa waathirika wa mafuriko wilayani Hanang’ mkoani Manyara, safari hii ikiwa ni mifuko ya saruji yenye thamani ya Sh.milioni 25.

Msaada huo umetolewa na kampuni ya BRAC Tanzania Finance Ltd (BTFL)
inayojihusisha na masuala ya kifedha imewakumbuka waathiriwa wa Mafuriko ya Katesh Hanang yaliyotokea Desemba mwaka jana.

Mafuriko hayo yaliweza kusababisha familia nyingi kukosa makazi na kukabiliwa na changamoto kubwa katika ujenzi wa nyumba zao pamoja na huduma zingine za kijamii.

Meneja wa Mawasiliano BTFL, Emma Mbaga, alisema wanalenga kuchangia zaidi katika ujenzi na kusaidia kupunguza
baadhi ya gharama inayowakabili waathirika wa mafuriko.

Alisema saruji ni nyenzo muhimu ya ujenzi ambayo itakuwa muhimu katika kujenga nyumba, miundombinu na maeneo ya huduma za kijamii ambavyo vimeharibiwa na mafuriko.

"Katika nyakati za shida, ni muhimu kwa mashirika na jamii kuja pamoja kushirikiana na kutoa msaada kwa wale wanaohitaji.

“Tulihuzunishwa sana na maafa na
uharibifu uliosababishwa na mafuriko na matope huko Katesh ambayo yameathiri wananchi wenzetu wengi,” alisema.

Makabidhiano ya mifuko 1,413 ya saruji yalifanyika katika Ofisi ya Wilaya ya Hanang’ mjini Katesh na mchango huo na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kateshi,
Janeth Mayenga.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya Janeth Mayenga, ameishukuru BTFL kwa kuwakumbuka wahanga wa mafuriko na kuwaletea saruji ambayo itawasaidia katika kujenga miundo mbini ambayo iliharibiwa.

Aidha, ameziomba taasisi zingine ziendelee kujitolea hata kwa kidogo kwani wananchi bado wanauhitaji mkubwa ili kurejea katika maisha yao kuwa kama hapo awali.

Brac Tanzania Finance Ltd (BTFL) imeendelea kujikita katika kusaidia jamii, ukiachilia mbali ni Taasisi ya kifedha ila imekua mstari wa mbele kutoa misaada kwa makundi mbalimbali.
 

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayenga (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Tawi na BRAC Tanzania Finance Ltd (BFTL) Lucy Mwaikena wakati wa makabidhiano ya mifuko ya saruji yenye thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko ya Katesh Hanang yaliyotokea mwezi Desemba mwaka jana.
 

Mkuu wa Wilaya ya Hanang Janeth Mayenga ( wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tawi la BRAC Tawi la Manyara wakati wa makabidhiano ya mifuko ya saruji yenye thamani ya Milioni 25 kwa ajili ya wananchi walioathirika na mafuriko ya Katesh Hanang yaliyotokea mwezi Desemba mwaka jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...