--Waungana kutoa msaada kwa Watoto na Wazee wenye uhitaji Hombolo
Katika kuelekea Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2024, Watumishi Wanawake wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wameungana kwa pamoja kutoa msaada kwa Watoto ambao wazazi wao wameshindwa kuwahudimia kutokana na hali ngumu ya maisha na Wazee walioshindwa kuhudumiwa na familia zao waliopo katika Kituo cha Masista cha Mother Teresa kilichopo Hombolo jijini Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya Wanawake wa GST wakati wakikabidhi msaada kituoni hapo, Meneja wa Rasilimali Watu na Utawala Jacqueline Kaluwa amesema, watumishi Wanawake wa GST wameona ni vyema kuanza kushehereke siku ya Wanawake Duniani kwa kuwashika mkono watoto na wazee wenye uhitaji wanao lelewa katika Kituo cha Mother Teresa.
Pamoja na mambo mengine, Kaluwa ameupongeza uongozi wa Kituo hicho kwa kuonesha nia na moyo wa kuwalea watoto na wazee hao na kuwaomba kuendelea na moyo huo wa kujitoa ili kuweza kuwasaidi wengi zaidi.
Kwa upande wake, Kiongozi wa Kituo hicho, Sister Marris amewapongeza Wanawake wa GST kwa kuonesha moyo wa kusaidia wenye uhitaji na kuwaomba kuendelea kuwa na moyo huo wa kujitolea.
Katika hatua nyingine, Sister Marris ametoa wito kwa taasisi zingine kuendelea kutoa misaada kwa lengo la kusaidia na kushiriki kuhudumia watoto, wazee na wengine wenye uhitaji.
Awali, Wanawake wa GST walipata fursa ya kupatiwa Elimu ya Afya ya Akili kutoka kwa Dkt. Japheth Swai wa Hospitali ya Mirembe ambaye hufundisha somo hilo kwa taasisi mbalimbali hususan katika kipindi cha kuelekea Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.
Elimu hiyo imetolewa Jijini Dodoma katika ukumbi wa Prof. Abdulkarim Mruma ambapo Wanawake wa Gst walipata nafasi ya kuuliza maswali na kujibiwa kwa ufasaha na Daktari huyo wa Afya ya Akili kutoka Hospital ya Mirembe Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...