Aidha,Andrea Isamaki Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ameshiriki kushuhudia Mafunzo,kiapo cha kutunza Siri na tamko la kujitoa uanachama kwa Makarani waongozaji
Nadia Issa na Benson Shawa,Makarani waongozaji wamesema wanakwenda kufanya kazi kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia Sheria,Kanuni na taratibu za Uchaguzi
Uchaguzi mdogo Kata ya Msangani unafanyika kutokana na kifo cha Mhe.Leonard Mlowe kilichotokea tarehe 23 Disemba,2023 ambapo jumla ya vyama nane (8) vya Siasa vinatarajia kushiriki.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...