Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba Commercial Bank (ACB) ametoa salaamu kwa Waislamu wote nchini na wateja wa benki hiyo popote walipo katika hafla ya Futari iliyoandaliwa kwa Wateja, Wafanyakazi pamoja na Wadau mbalimbali wa benki hiyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Akizungumza Katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 25, 2024 katika Hoteli ya Serena Bw. Silvest Arumasi ametumia fursa hiyo kuwapongeza Waislamu wote kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na amewashukuru wadau wote kwa kutenga muda wao na kujumuika pamoja katika Futari hiyo kwani kwa kitendo hicho kimeleta faraja na heshima kubwa sana.

Aidha, alisema kuwa, ACB imekuwa na utamaduni wa kufanya hafla ya kufuturisha kwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono ndugu zetu Waislam katika funga yao na pia ni njia nzuri ya kuboresha mahusiano ya benki na wateja wake.

Akiba Commercial Bank inatambua na kuheshimu sana Imani za wateja, Wafanyakazi na wadau wake na kuupa umuhimu wa kipekee mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Bw. Silvest Arumasi amesema kuwa ACB inaendelea kuboresha na kupanua wigo wa huduma zake ili kuendana na soko kwa lengo ya kukidhi matarajio ya wateja, amewaomba wateja na umma kwa ujumla kuendelea kuiamini Benki hiyo ambayo imeweza kuwahudumia Watanzania wengi na kuleta maendeleo makubwa kwa wajasiriamali na Jamii nzima kwa ujumla.

Akiba Commercial Bank Benki kwa maendeleo yako

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...