Njombe
WAKATI wanafunzi wa kidato cha sita wakitarajia kufanya mtihani wao wa mwisho mwezi Mei mwaka huu,Wahitimu wametakiwa kuzingatia maadili,Nidhamu na weledi mkubwa pamoja na kumtanguliza mungu.

Katika mahafali ya Kidini ya Wanafunzi wa Dhehebu la Roman Katholi TYCS kidato cha sita kwa shule za sekondari Njombe(NJOSS) Uwemba na Wanike yaliyofanyika Njoss Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amewataka wahitimu hao kutambua kuwa utovu wa nidhamu unasababishwa na kutokuwa na Imani thabiti.

Aidha Mpete ameonya dhidi ya mmomonyoko wa maadili unaochagiza kuwapo kwa mapenzi ya jinsi moja huku akiwataka walimu kuwaacha wanafunzi wasome badala ya kuwarubuni.

"Mtumie fursa hiyo ili tuepukane na mapenzi ya jinsia moja lakini mbaya zaidi kumekuwepo na tabia ya sisi watu wazima kuwahadaa hawa watoto niwaombe kama mtakutana na changamoto za namna hiyo msisite na mtoe taarifa"amesema Mpete

Katika taarifa ya wahitimu hao iliyosomwa na Joachim Shayo imeeleza kuwa nidhamu ndio nguzo ya mafanikio yao na kwamba wamekuwa wakifanya vyema katika mitihani kutokana na Kuzingatia maadili mema.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa shule ya sekondari Njombe makamu wa shule hiyo Mwalimu Melkisedeck Mbata amewataka wanafunzi kwenda kufanyia kazi nasaha zilizotolewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...