Na Jacquiline Mrisho – Maelezo

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka amesema kuwa ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa unaoendelea katika eneo la Kilimani mkoani Dodoma.

Ameyasema hayo leo Machi 13, 2024 jijini Dodoma wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kutembelea mradi huo ili kukagua maendeleo ya ujenzi na kupata taarifa ya matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya mradi huo.

“Ujenzi unaendelea vizuri na tumejionea kuwa umejengwa kwa ubora na viwango vinavyotakiwa, vifaa vya kuendeleza ujenzi vipo vya kutosha, tumeona kuwa thamani ya fedha iliyotumika hadi sasa inaakisi ukubwa wa kazi iliyofikiwa, tunaamini kazi hii itakamilika kwa viwango sahihi”, alisema mheshimiwa Naghenjwa.

Akisoma taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo mbele ya kamati, Mshauri Mwelekezi kutoka Chuo Kikuu Ardhi, Mhandisi Denatus Dominick amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 20.4 ambapo fedha hizo zimetumika kujenga jengo la ghorofa sita lenye vyumba vya ofisi 115, kumbi za mikutano 7, ukumbi wa chakula mmoja, maktaba moja, uzio, sehemu za maegesho ya magari, mfumo wa majitaka, tanki la kuhifadhia maji, mifumo ya umeme na bustani.

“Mpaka sasa mradi huu umetekelezwa kwa takriban asilimia 84 kwa kazi ya jengo kuu na kazi za nje na asilimia 30 kwa kazi za mifumo ya umeme na mitambo. Mradi huu umetumika kama sehemu ya mafunzo kwa vijana wa vyuo mbalimbali wanaokuja kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo, umetoa ajira za muda mfupi kwa wazawa na mradi utakapokamilika utaongeza mapato kwa serikali kupitia ukodishaji wa kumbi zilizopo kwenye jingo hili”, alisema Dominick.

Amemaliza kwa kusisitiza kuwa mradi huo unatekelezwa kwa kuzingatia ubora na kuahidi kuwa watajitahidi kusimamia mradi huo kwa uadilifu ili kumaliza mradi huo kwa wakati.
Thumbnail 2: Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi (mwenye kaunda suti nyeusi) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali walipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa unaoendelea eneo la Kilimani, jijini Dodoma. (Picha na ORPP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...