Na Saidina Msangi na Joseph Mahumi, WF, Dodoma
Waziri
 wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), amesema kuwa Tanzania 
ni nchi ya mfano Afrika kwa kutimiza viashiria vya Malengo ya Milenia 
ambapo imefanya vizuri katika sekta za Afya, Elimu, Maji. 
Dkt.
 Nchemba alitoa ufafanuzi huo wa ukomo wa Bajeti kwa mwaka 2024/25, 
wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi katika jengo la Taaluma la Chuo 
cha Uhasibu Arusha (IAA), jijini Dodoma.
Alisema
 kuwa katika makadirio yaliyowasilishwa bungeni Serikali inatarajia 
kutumia kiasi cha shilingi trilioni 49.34 ambapo fedha za maendeleo 
zilizotengwa ni kiasi cha shilingi trilioni 16.
‘‘Fedha
 za maendeleo ni trilioni 16, fedha hizi zinatarajiwa kutumika katika 
Miradi ya Kilimo cha Umwagiliaji, Elimu ya Msingi na Elimu ya Juu, 
Ujenzi wa Barabara, Maji, Umeme Miradi ya Afya pamoja na ukamilishaji wa
 Bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere’’, alifafanua Dkt. Nchemba.  
Alisema
 kiasi cha fedha kinachotarajiwa kutumika katika uchaguzi ni shilingi 
bilioni 600 kwa mwaka unaofuata na kwa mwaka huu ni Shilingi bilioni 300
 inayoenda kwenye uchaguzi.
‘‘Uchaguzi
 ni matakwa la kikatiba sio maamuzi ya Serikali bali ni kuhakikisha kuwa
 matakwa ya kikatiba yanatimizwa hivyo katika bajeti ya Sh. trilioni 49 
kiasi kitakachoitumika katika kuendesha uchaguzi kwa mwaka ujao ni 
shilingi bilioni 300, alifafanua Dkt. Nchemba.
Akifafanua
 kuhusu fedha zinazotarajiwa kutumika katika maandalizi ya Kombe la 
Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 linalotarajiwa kufanyika Tanzania Dkt. 
Nchemba alisema kuwa Tanzania kuwa mwenyeji wa AFCON ni suala la 
kujivunia kwani ni heshima kwa Taifa ambapo kiasi kilichotengwa ni Sh. 
bilioni 200 tu katika bajeti ya shilingi. trilioni 49. 
Akizungumza
 kuhusu ugharamiaji wa Deni la Taifa Dkt. Nchemba alisema kuwa katika 
sh. trilioni 49, deni halisi ni shilingi trilioni tano (5) pamoja na 
riba ambayo haitazidi kiasi cha shilingi trilioni 10. 
‘'Deni
 lenyewe ni miradi ya maendeleo inayoonekana kama ni ujenzi wa reli ya 
kisasa, kivuko cha Kigongo Busisi Mwanza, ujenzi wa mabweni ya shule, 
tumejenga mabweni ya vyuo vikuu karibu kila chuo kimepata kwa mradi 
mkubwa wa fedha za Benki ya Dunia ili kuwawezesha wanafunzi wakae katika
 mazingira salama’’,
alifafanua Dkt. Nchemba.
Aliongeza
 kuwa jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita zinaonekana kwani fedha za 
maendeleo yanayotekelezwa yanajitambulisha kwani zimegusa mpaka kwenye 
maeneo ambayo hayajawahi kupata maendeleo.
‘‘Vijiji
 ambavyo havijawahi kupata barabara sasa vina madaraja na barabara 
kuunganisha vijiji na sasa zinaenda kujengwa barabara za kudumu, vituo 
vya afya vimejengwa kwenye kila makao makuu ya tarafa pamoja na kuweka 
vitendea kazi ambapo ndani ya miaka mitatu mikoa yote ina CT SCAN ambapo
 awali zilikuwepo 6 nchi nzima’’, alifafanua Dkt. Nchemba. 
 Waziri
 wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza 
wakati wa hafla ya Uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma 
la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Kampasi ya Dodoma, katika eneo la 
Njedengwa, jijini Dodoma, ambapo alitumia jukwaa hilo kufafanua ukomo wa Bajeti kwa mwaka 2024/25.


 

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...