Kamishina  wa  Uhifadhi wa Shirika la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) Mussa Kuji akizungumza   Mafanikio ya TANAPA katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mheshimwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kikao kazi na Wahariri wa vyombo vya Habari kilichofanyika chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile akizungumza kuhusiana na umhimu wa waandishi kutumika kalamu katika kutangaza hifadhi zetu weledi.
Afisa Habari Mwandamizi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabatho Kosuri, akizungumza kuhusiana na vikao kazi kati ya Taasisi zilizochini ya Msajili wa Hazina ,jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika mkutano wa TANAPA  na wahariri na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam.

*Kamishina Kuji na timu yake aweka mikakati ya kung'arisha TANAPA

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
SHIRIKA la Taifa la Uhifadhi (TANAPA) limesema kuwa limepata mafanikio hifadhi za Taifa kutembelewa kwa idadi kubwa ya watalii hadi kufikia2024 idadi ya watalii 1,514,726 kutokana na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendelea kuliwezesha Shirika kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa

Hayo ameyasema Kamishina Mkuu wa Uhifadhi Mussa Kuji wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kuhusiana na mafanikio ya Shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina jijini Dar es Salaam.

Kamishina Kuji amesema kuwa mafaniko hayo yameongeza mapato na hii inatokana na Filam ya Royal Tour aliyoifanya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuingia mwenyewe hifadhin hali inayoonesha kuwa kuna uongozi mahiri kuimarisha na kukuza sekta ya uhifadhi na utalii nchini katika kipindi chake cha uongozi wa nchi kwa miaka hii mitatu.

Amesema katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 – Machi 19, 2024 idadi ya watalii 1,514,726 (wa ndani wakiwa 721,543 na wa nje wakiwa 793,183) wametembelea Hifadhi za Taifa sawa na ongezeko la asilimia 5

“Mafanikio haya yanayoendelea kufanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa ushiriki wake wa moja kwa moja kwenye kukuza sekta ya uhifadhi wa wanyamapori na utalii ikiwemo ushiriki wake kwenye filamu maarufu ijulikanayo kama “Tanzania: The Royal Tour”. Filamu hii imeleta chachu kubwa katika ukuaji wa utalii hapa nchini nchini pamoja na kuendelea kuelekeza fedha katika sekta ya uhifadhi na utalii”amesema Kuji .

Amesema Shirika linasimamia Hifadhi za Taifa 21 zenye eneo la ukubwa wa kilomita za mraba 96,908.88 ambalo ni sawa na 10.2% ya eneo lote la nchi.

Aidha amesema kuongezeka kwa idadi ya watalii katika Hifadhi za Taifa kumekuwa na ongezeko la watalii wanaotembelea Hifadhi za Taifa katika mwaka 2018/2019 jumla ya Watalii waliotembelea Hifadhi za Taifa walikuwa watalii 1,452,345 ikihusisha watalii wa ndani (719,172) na nje (733,173).

Hata hivyo amesema idadi ya watalii ilipungua hadi kufikia 485,827 mwaka 2020 ambayo ilitokana na UVIKO-19.

Mwaka 2021/2022 idadi ya watalii ilianza kupanda na kufikia watalii 997,87 nq 2 Hali ya kuimarika kwa utalii nchini iliendelea kupanda ambapo mwaka 2022/2023 idadi ya watalii waliongezeka na kufikia 1,670,437.

Aidha, kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024 katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 – Machi 19, 2024 idadi ya watalii 1,514,726 (wa ndani wakiwa 721,543 na wa nje wakiwa 793,183) wametembelea Hifadhi za Taifa sawa na ongezeko la asilimia 5 ikiwa ni zaidi ya lengo la kupokea watalii 1,387,987 (wa nje 827,713 na watalii wa ndani 726,676) katika kipindi husika.

Aidha, idadi ya watalii wanaotarajiwa kutembelea Hifadhi za Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ni 1,830,081 (watalii wa nje 963,413 na watalii wa ndani 866,667).

Amesema katika kipindi cha miaka mitatu kumekuwepo na ongezeko la siku za kukaa wageni kutoka wastani wa siku 1,749,194 katika mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia wastani wa siku 2,669,586 kufikia Februari 2024 ambalo ongezeko hilo limechangia mapato.

Amesema Katika kipindi cha miaka mitatu, kumekuwepo na ongezeko la mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 174 (2021/2022) hadi kufikia zaidi ya shilingi bilioni 337 kwa mwaka 2022/2023 sawa na ongezeko la shilingi zaidi ya bilioni 162 ambayo ni asilimia 94.

Aidha, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 (Julai 2023 hadi Machi 19, 2024) Shirika limekusanya zaidi shilingi Bilioni 340 ukilinganisha na matarajio ya kukusanya zaidi shilingi bilioni 295 mpaka Machi 2024. Kiasi hiki (Bilion 340) ni ongezeko la zaidi ya shilingi ya bilioni 44 ambayo ni sawa na asilimia 15 huku Shirika lina matarajio ya kukusanya kiasi cha zaidi shilingi bilioni 382 hadi Juni 2024.

Mapato haya ya sasa yanazidi mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 282 yaliyokusanywa mwaka 2018/2019 kabla ya janga la UVIKO – 19 ambayo yalikuwa ndio kiwango cha juu cha mapato katika Shirika.

Kamishina Kuji amesema kuwa kumekuwepo na kuchipuka kwa masoko mapya ya utalii yenye idadi kubwa ya watalii ambapo inatoa uhakika wa kuendelea kupokea watalii wengi kuja kutembelea Hifadhi za Taifa.

Amesema TANAPA imefanikiwa kupata tuzo ijulikanayo kama “Best Practice Award” ambayo hutolewa kila mwaka na taasisi ya “European Society for Quality Research - ESQR”. Tuzo hii ya utoaji wa huduma bora kimataifa hutolewa na taasisi hiyo baada ya kutambua taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali pamoja na watu binafsi wanaotoa huduma za ubora wa viwango vya hali ya juu kimataifa.

TANAPA imeendelea kupata tuzo zinazotolewa na taasisi ya ESQR kwa kipindi cha miaka minne (4) mfululizo ambazo kati ya hizo tuzo za miaka mitatu (3) mfululizo zimepatikana katika kipindi cha uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita kwa kiwango cha “Platinum category” mwaka 2021, “Gold category” mwaka 2022 na “Diamond category” mwaka 2023.

Kamishina huyo amesema Hifadhi ya Taifa Serengeti imepata tuzo itolewayo na shirika la “World Travel Awards (WTA)” ya kuwa hifadhi bora barani Afrika kwa miaka mitano mfululizo (2019 hadi 2023). Tuzo tatu (3) kati ya hizo tano (5) zimepatikana chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita (tuzo za mwaka 2021 hadi 2023).

Hifadhi ya Taifa Tarangire na Kilimanjaro zilipata tuzo mara mbili mfululizo kwa mwaka 2021 na 2022 ya kuwa vituo vyenye mvuto katika utalii na Tuzo hizo hutolewa na jukwaa la kimataifa lijulikanalo kwa jina la “Trip Advisor”.

Pia, kampuni ya Explore Worldwide yenye makao yake makuu nchini Uingereza mwaka huu 2024 imeutambua Mlima Kilimanjaro kuwa namba moja ya Alama za Asili za kudumu na zinazokumbukwa zaidi ulimwenguni (World’s topmost unforgettable natural landmarks).

Amesema Tuzo hizo zimeliongezea Shirika kuaminiwa na wateja mbalimbali na kutoa uhakika kwao kuhusu aina ya huduma zitolewazo, kutambulika zaidi na kuongeza idadi ya watalii pamoja na kutoa uhakika kwa watalii na wadau wa utalii kuhusu ubora wa hifadhi.

Amesema katika mafanikio hayo ni pamoja na kuwepo na ongezeko la wawekezaji kwenye maeneo ambayo yaliyokuwa hayana mvuto kwa wawekezaji zikiwemo Hifadhi za Ruaha, Saadani na Mikumi ikiwa na Jumla ya maeneo mapya ya uwekezaji 176 (34 ni loji na 142 ni kambi) yameainishwa katika Hifadhi zote kwa kuzingatia mipango ya uendeshaji wa kila Hifadhi na yametangazwa kwenye tovuti ya Shirika.

Amesema kuongezeka kwa wigo wa shughuli za utalii wa puto (balloon) kutoka kufanyika katika Hifadhi ya Taifa Serengeti kwenda hifadhi za Tarangire, Ruaha na sasa maandalizi yanaendelea kwa hifadhi ya Mikumi; Utalii wa faru (Hifadhi ya Taifa Mkomazi), utalii wa baiskeli (Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro na Arusha.

Mwaka 2018 TANAPA iliingia katika mchakato wa kutambuliwa na Shirika la Viwango Duniani ili kujijengea kuaminiwa na wateja. Kutambuliwa kwa TANAPA mwaka 2021 na ISO kumepelekea wateja kuamini na kuchagua huduma zinazotolewa na TANAPA na hifadhi zake hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato. Katika miaka mitatu, Shirika limeendelea kutekeleza shughuli za utalii na uhifadhi kwa kuzingatia matakwa ya kiwango cha ubora cha ISO 9001:2015 kinachohusu utoaji wa huduma bora kwa wateja.

TANAPA imeendelea kuimarisha miundombinu ya ukusanyaji wa mapato ikiwemo kukamilisha ujenzi wa lango la kisasa la Naabi lenye uwezo wa kupokea zaidi ya magari 600 na wastani wa wageni zaidi ya 1,500 kwa siku. Katika kipindi cha miaka mitatu TANAPA pia imeweza kujenga malango mapya 10 na ya kisasa katika Hifadhi za Taifa Tarangire (2), Mkomazi (3), Serengeti (2) na Nyerere (3).

kutambua mienendo yao ili kurahisisha udhibiti wanapotoka nje ya maeneo ya hifadhi.

Hata hivyo amesema kupitia mradi wa REGROW, Shirika limewezesha mafunzo kwa askari wa vijiji (Village Game Scout – VGS) 354 kutoka vijiji 39 ili kuwezesha kukabili kwa wakati matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Aidha, Shirika linaendelea na ujenzi wa vituo 8 vya Askari Uhifadhi katika maeneo ya kimkakati yaliyopo katika vijiji vinavyoathirika zaidi katika wilaya za Mbarali, Kalambo, Kilwa, Namtumbo, Ruangwa, Serengeti, Bunda na Bariadi. Vituo hivi vitasaidia askari kudhibiti kwa wakati wanyamapori wakali na waharibifu.

Shirika limeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuhakikisha kuwa linabuni vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vitaliingizia Shirika fedha na kuongeza ukusanyaji wa mapato. Miongoni mwa vyanzo bunifu vya mapato ambavyo vimeendelea kuibuliwa na Shirika ni pamoja na kuanzishwa kwa Kampuni Tanzu ya Uwekezaji ya Shirika (TANAPA Investment Limited – TIL) inayolenga kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa miradi ya kimkakati na pia kuwa chanzo kikubwa cha mapato kwa Shirika kwa kutekeleza miradi mbalimbali Kuanzishwa kwa Kiwanda cha Ushonaji wa sare za watumishi na kupokea zabuni kutoka taasisi nyingi

Ujenzi wa Hoteli yenye hadhi ya nyota tatu katika eneo la Rubambagwe Wilaya ya Chato yenye vyumba 30 vya kulala; na Ujenzi wa Uwanja wa Gofu wa hadhi ya kimataifa wenye mashimo 18 uliopo eneo la Forti Ikoma - Hifadhi ya Taifa Serengeti.

Shirika limeendela kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori walio katika hatari ya kutoweka na kuwezesha kuongezeka kwa idadi ya Wanyama hao wakiwemo faru, mbwa mwitu na sokwe.

Serikali ya awamu ya sita (6) imeweka mazingira wezeshi kwa Shirika kusimamia maliasili zilizopo katika Hifadhi za Taifa hapa nchini pamoja na upatikanaji wa rasimilimali fedha, rasilimali watu na vitendea kazi kama magari, mitambo ya kutengeneza barabara na mafunzo kwa watendaji.

Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na Kudhibiti uwindaji wa wanyama adimu ambapo hakukuwa na tukio la kuuawa kwa Faru, Sokwe au Mbwa mwitu.

Amesema kuwa wamekuwa na jitihada za kudhibiti uingizwaji wa mifugo hifadhini kwa kufanya doria na kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii zinazoishi jirani na hifadhi. Madhara ya uingizaji wa mifugo ni pamoja na uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji, maambukizi ya magonjwa kutoka kwa wanyama wafugwao kwenda kwa wanyamapori, kuendelea kushamiri na kusambaa kwa mimea vamizi na kuharibu shughuli za utalii.

Amesema Shirika linakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo Mabadiliko ya tabia nchi; (ukame, mafuriko, uwepo wa mimea vamizi inayoathiri upatikanaji wa chakula na mizinguko ya wanyamapori, uwepo wa ujangili ,Matukio ya uingizwaji wa mifugo ndani ya hifadhi,Matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu katika maeneo ya jamii.

Shirika limeendelea kujiimarisha katika jitihada za utatuzi wa changamoto miongoni mwa mikakati inayoendelea kutekelezwa kama sehemu ya kukabiliana na baadhi changamoto zilizopo za uhifadhi na utalii ni pamoja Kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...