HATIMAYE Chama cha Tanzania Labor Party (TLP) kinatarajia kufanya mkutano Mkuu Maalumu wa kujaza nafasi Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Machi 27 Mwaka huu baada ya 'vuta nikuvute' ndani ya chama hicho ya muda mrefu.

Akithibitisha kufanyika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu wa Chama hicho Damaly Richard amesema hatua hiyo imekuja baada ya kukamilisha maelekezo ya Ofisi Msajili wa Vyama vya Siasa na Katiba ya TLP huu ya namna ya kufanya uchaguzi huo unaotarajiwa kuziba pengo la aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Hayati Agustino Lyatonga Mrema.

"Uchaguzi huu tunaufanya hasa baada ya kukamilika kwa maagizo ya kiutaratibu ambayo Ofisi ya Msajili a Vyama vya Siasa ilitupatia kuruhusu uchaguzi uweze kufanyika, hadi sasa kila kitu kimekwenda sawa kilichobaki ni kufanyika kwa uchaguzi huo" amesisitiza Damaly

Amesema kutokana na maamuzi hayo, Kamati imewaandikia barua za kuwataarifu wajumbe wote kuhusu tarehe ya uchaguzi huku ikiwataka kujiandaa na uchaguzi, na kutokanana na hatua ya wajumbe kujigharamia nauli wenyewe kamati inaendelea na taratibu za kutafuta uwezeshaji wa sare, kofia na posho kwa ajili ya kuwapunguzia gharama wajumbe hao.
"Tunawaomba wajumbe wwa mkutano Mkuu kushiriki ili kumchagua Mwenyekiti wa Chama Taifa wakati huu tunapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa pamoja na uchaguzi Mkuu hapo Mwakani" amesisitiza Mwenyekiti huyo

Kuchelewa kufanyika kwa uchaguzi huo hasa baada ya kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wake Hayati Mrema kulitokana na vuta nikuvute ya baadhi ya viongozi wa chama hicho ikidaiwa kuwa mmoja wa viongozi hao ambaye pia alichukua fomu ya kugombea nafasi ya uenyekiti kutaka kujiwekea mazingira ya yeye kushinda akiingiza taratibu ambazo hazimo kikatiba.

Hatua hiyo iliyopelekea mvutano baina ya viongozi pamoja na wanachama wa TLP hadi malalamiko kuifikia Ofisi ya Msajili, ndiyo hasa sababu ya kuchelewa kufanyika kwa uchaguzi huo hadi pale Ofisi ya Msajili ilipotoa taratibu zingine za kuzifuata kwa ajili ya kuwezesha uchaguzi huo kufanyika.

"Tunawashukuru wanachama kwa uvumilivu wao kwa kipindi chote ambacho chama kimepita kipindi kigumu na sasa tunaomba tena kukiombea Chama ili tuweze kujaza nafasi ya Mwenyekiti Taifa tayari kwa maandalizi ya kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa vyama vyote hapo Mwakani" amesisitiza Damaly

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...