TIGO  yachaguliwa kuwania Tuzo ya ITU WSIS 2024 Kupitia mradi wa UCSAF (Mfuko wa mawasiliano kwa wote)-Zanzibar

Mradi wa Tigo wa Mawasiliano ya Vijijini huko Zanzibar, kwa ushirikiano na UCSAF umependekezwa kuwania Tuzo za ITU WSIS 2024.

Mradi huo umechaguliwa baada ya kufanikiwa kushughulikia changamoto za mawasiliano kwa kutambua maeneo 42 katika kata 38 kwa kupitia Serikali. Tigo Zantel, kama mtoa huduma mmoja wa pekee, walikamilisha mradi huo kwa muda wa takriban chini ya mwaka mmoja ambapo watu 211,601 wamenufaika na mradi huu.

Ninawasihi nyote mpigie kura mradi wetu ili kushinda tuzo hii ya kimataifa yenye heshima kwa kufuata hatua rahisi zifuatazo:

Hatua 1: Bonyeza kwenye URL ifuatayo: https://www.itu.int/net4/wsis/stocktaking/Prizes/2024 Hatua 2: Bonyeza kitufe cha Piga Kura na tengeneza akaunti mpya. Hatua 3: Kwenye menyu kuu, Chagua Kura Hatua 4: Chini ya WSIS 2024, Chagua AL C2. Miundombinu ya Habari na Mawasiliano Hatua 5: Futa chini na piga kura kwa "MRADI WA MAWASILIANO YA VIJIJINI HUKO ZANZIBAR".

Upigaji kura unafungwa tarehe 31 Machi 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...