Na Said Mwishehe,Michuzi TV

NCHI zaidi ya 50 zinatarajia kushiriki katika Kongamano la 10 la Jotoaridhi Afrika(ARGeo-C10) linalotarajia kufanyika Novema mwaka huu ambapo Tanzania tayari imezindua maandalizi ya kuandaa Kongamano hilo linalotarajia pia kushirikisha wadau mbalimbali.

Akizungumza leo Machi 18,2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa Tanzania ikizindua maandalizi ya Kongamano hilo, Kamshina wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga amesema Kongamano hilo litafanyika kuanzia Novemba 11 hadi Novemba 17 mwaka huu 

Akifafanua zaidi ameeleza kwamba nchi 50 zikiwemo wanachama wa ARGeo ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia na Djibout zitashiriki na washiriki watakaohudhuria ni zaidi ya watu 1000.

"Katika kongamano hilo zaidi ya watu 1,000 wa kada mbalimbali zinazohusiana na sekta hiyo muhimu katika kuzalisha nishati safi na salama wanatarajiwa kushiriki."

Akieleza zaidi Mhandisi Luoga amesema mwaka 2022 Rais Dk.Samia Suluhu Hassan alikubali ombi la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) kufanyika kwa kongamano hilo, hivyo kwa sasa Tanzania inaendelea na maandalizi ili liweze lifanye na leo ndio umefanyika uzinduzi rasmi wa maandalizi ya Kongamano hilo.

Ameongeza Serikali kupitia Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) itashirikiana na UNEP kuhakikisha kongamano hilo muhimu linafanikiwa kwa kiwango kikubwa, ili dhamira ya serikali kuongeza nishati jadidifu inafikiwa.

Pia amesema kongamano hilo ni muhimu kwa Tanzania kutokana na kuwa na rasilimali nyingi za jotoardhi, hivyo matumaini yao ni kuwa washiriki wataweza kujifunza na kubadilishana taaluma.

"Tunatarajia wataalam, wawekezaji, wafanyabiashara na viongozi mbalimbali ambao watashiriki Kongamano hilo la Jotoaridhi watapata nafasi ya kuchochea kasi ya uzalishaji nishati hii kupitia majadiliano na maazimio yatakayotolewa wakati wa Kongamano."

Kuhusu rasilimali ya jotoaridhi, Mhandisi Luoga amesema ulianza kufanyiwa utafiti tangu mwaka 1970 hivyo kwa sasa wanaendelea na utekelezaji wa kuzalisha kupitia TGDC ambapo wameanza kwenye baadhi ya maeneo kati ya 51 yanayoweza kuzalisha nishati hiyo.

"Kwa mujibu wa tafiti zilizopo zinaonesha Tanzania inaweza kuzalishaji megawati 5,000 za umeme wa jotoardhi na tunaendelea kutekeleza miradi ambayo inatarajiwa kuzalisha megawati 200 ifikapo mwaka 2027."

Aidha amesema kuna maeneo matano ambayo tumeyaainisha kwa ajili ya uzalishaji wa nishati ya jotoardhi ambayo ni Ngozi(megawani 70), Kiejo Mbaka(megawati 60) , Natron (megawati 60), Songwe (megawati tano)na Ruoyi Kisaki (megawati tano) hadi kufikia megawati 200.

Kwa pande wake Meneja wa TGDC, Mhandisi Mathew Mwangomba amefafanua kongamano hilo la 10 ambalo litafanyika nchini Tanzania limekuja wakati muafaka kwania dunia ipo katika mapambano ya kupunguza hewa ukaa ambayo imekuwa na madhara makubwa kwenye mazingira na kuongeza Nishati itokanayo na Jotoaridhi ni rafiki wa mazingira.

Pia amesema upatikanaji wa jotoardhi nchini unaendana na hatua tatu muhimu ambazo ni sayansi jiolojia, jiofizikia na jiokemia ambayo ipo nchini kupitia Bonde la Ufa la Magharibi, Mashariki na Kusini ambayo kitalaam wanaiita Tripple Juction.

Ameeleza pia  TGDC wanatekeleza Ngozi kuchimba nishati ya jotoardhi ambayo inapatikana kwa nyuzi joto 250, hivyo basi kukutana kwa wadau 1,000 kujadili jotoardhi tunaenda kupiga hatua zaidi,” alisema.

Awali Mwakilishi Mkazi wa UNEP Tanzania, Clara Makenya  amesema kwamba wanatarajia kongamano hilo litatoa mwanga kwa duania kuwekeza katika nishati safi na salama kama jotoardhi na kuachana na nishati ambazo zina madhara kwa jamii na mazingira.





Uzinduzi wa kongamano la jotoardhi la kikanda Afrika ambalo linatarajiwa kufanyika Novemba 11 hadi 17, 2024  katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam, ambapo washiriki zaidi ya 600 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo, ni mara ya pili Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo uliofanyika 2014 jijini Arusha kwa mara ya kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...