Na Yeremias Ngerangera ....Namtumbo.
PAMOJA na Hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali kuhusu kukomesha ukatili wa kijinsia ,wanawake Wilayani Namtumbo wametumia Maadhimisho ya wiki ya kuelekea kilele Cha siku ya wanawake Duniani kupaza sauti zao kulalamikia ukatili wa kijinsia.

Kwa Mujibu wa Risala ya wanawake wa Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Kwa mgeni Rasmi Ngollo Malenya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo wanawake hao wameendelea kulalamikia matendo ya ukatili wa kijinsia hasa Kwa wanawake waishio vijijini.

Risala iliyosomwa na Loema Thomas Safari ilitamka bayana kuwa wanawake Wilayani humo bado wanafanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kunyanyaswa, kukandamizwa, kufanyiwa vitendo viovu visivyostahili Kwa binadamu.

Aidha katika taarifa hiyo imeeleza kuwa wanawake wa vijijini Wilayani humo hunyimwa uhuru wa kutoa maamuzi kuhusu kupanga matumizi ya mapato yatokanayo na mazao waliyolima,kufanyishwa kazi Bila kupumzika ,kupigwa na hata kufukuzwa kwenye ndoa na pengine kunyang'anywa Mali.

Kwa Mujibu wa wanawake hao walisema kutokana na matendo hayo ya ukatili familia nyingi huwa duni kiuchumi ,familia kufarakana ,kupotea Kwa amani katika familia na kusababisha watoto wa mitaani na vijana kuzagaa mijini na mwishowe hujikita katika vitendo visivyokuwa vya kimaadili .

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Peres Kamugisha pamoja na kuwapongeza wanawake wa Wilaya ya Namtumbo Kwa kuazimisha siku ya wanawake kiwilaya aliitaka Jamii kuwekeza katika watoto wa kike akiamini kuwekeza Kwa mtoto wa kike Kuna faida kubwa.

Kamugisha aliwaambia wanawake kuwa katika Nchi yetu wanawake wamedhihirisha kuwa ni viongozi thabiti na mahiri kuanzia kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwanamke ,viongozi wengine wanawake waliopewa nyadhifa mbalimbali wanaonesha kumudu vyema nafasi zao alisema Kamugisha.

​Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Ngollo Malenya pamoja na kumshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kuwawezesha wanawake kwa kuwapa mikopo kupitia mfuko wa maendeleo Kwa wanawake wenye thamani ya shilingi 287,680,000 toka mwaka 2015 mpaka mwaka 2024 alisema Serikali ya awamu ya Sita imedhamiria kuwaondolea Changamoto wanawake Kwa kufanikisha kujenga vituo viwili vya afya ,Ligera na Magazini ambavyo vimewaondolea wanawake Changamoto za upatikanaji wa huduma za afya hasa akina mama wajawazito.

Pamoja na hayo Malenya aliwaambia wanawake hao kuwa Nchi yetu imepiga hatua Mbele kwani imeshika namba 53 kati ya Nchi 144 zinazofanya vizuri katika masuala ya kijinsia kadiri ya taarifa jukwaa la uchumi Duniani kuhusu pengo la jinsia la mwaka 2016.

Malenya aliongeza Serikali imekamilisha ujenzi wa Sekondari ya Kisasa ya wasichana katika Wilaya yetu iliyogharimu shilingi 4,500,000,000 ili kuwawezesha watoto wa kike kupata elimu Bora.

Hata hivyo Malenya aliwataka wanawake wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi Kwa kuwa ni haki Yao kikatiba huku akiwahatarisha kujihadhari na ugonjwa wa ukimwi.

Awali Maadhimisho hayo yalianza Kwa Mgeni Rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo kugawia taulo za kike wanafunzi wa kike wa shule za msingi, sekondari Pamoja na chuo Cha ufundi stadi (VETA) zenye thamani ya shilingi milioni 2.

Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo Kwa mwaka huu ni "Wekeza Kwa wanawake Kuharakisha maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...