Imeelezwa kwamba watumishi wanawake wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) nchini wana mchango mkubwa katika kufanikisha utekelezaji wa majukuu ya Taasisi hiyo.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TARURA Bi. Azmina Mbilinyi wakati wa sherehe za pamoja kwa watumishi wanawake ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma

“Nawapongeza wanawake wote na kuwatia moyo kwamba tunatambua mchango wenu mkubwa mnaofanya katika kuhakikisha utekelezaji wa kazi za taasisi unafanikiwa”.

Amesema anatamani wanawake hao siku moja wawe viongozi wakubwa na wengine kuwa ni mameneja TARURA ama sehemu nyingine katika utumishi wao.

“Chapeni kazi kwa msaada wa Mungu mnaweza kufanya mambo makubwa wote mnaweza “.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi huyo aliwaasa wanawake hao kutumia muda wao katika kuangalia familia licha ya muda mwingi kuwepo kazini.

“Hivi sasa yapo matatizo makubwa sehemu tunazoishi ikiwemo unyanyanyasi wa watoto, kwa hiyo pamoja na majukumu mengi mliyonayo kazini mnapaswa pia muangalie familia zenu katika makuzi na malezi kwa watoto wetu ili waje kuwa baba na mama bora hapo baadae”alisisitiza Bi. Azmina

Hata hivyo aliwashauri wanawake hao kuwekeza baadhi ya mifuko ya uwekezaji pamoja na kuthubutu kwa kuanzisha biashara ambazo zitawaongezea vipato vya ziada.

Sherehe hiyo ilihudhuriwa na watumishi wanawake kutoka TARURA Makao Makuu pamoja na ofisi za mameneja wa Mikoa na Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...