Na.Abel Paul, Jeshi la Polisi- Igunga Tabora.

Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo limesema litaendelea kutoa elimu kwa wafugaji na wafanya biashara wa Mifugo hapa Nchini huku likibainisha kuwa halitomwonea muhali mfugaji yeyote atakaye bainika kutorosha mifugo na kukiuka taratibu za uuzaji wa mifugo hapa nchini.

Hayo yamebainisha leo Machi 09, 2024 Wilaya ya Igunga Mkoa wa Tabora na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo hapa nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua alipotembelea mnada wa Upili Igunga ambapo amebainisha kuwa kikosi hicho kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji Nchi nzima ili kuondokana uvunjifu wa sheria.

SACP Pasua ameongeza kuwa wafugaji hapa nchini wanatakiwa kufuata taratibu za uuzaji wa Mifugo yao ambapo amesema watakao kiuka taratibu hizo kikosi cha kuzuia wizi wa Mifugo kitaendelea kuwachukulia hatua za kisheria ikiwa ni Pamoja na kuwafikisha Mahakamani wale wote watakao bainika kuvunja sheria.

Aidha ametoa wito kwa wananchi kote Nchini kuendelea kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi za baadhi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo ili hatua sitahiki zichukuliwe kwa watao bainika kujihusha na uhalifu huo hapa nchini.

Baadhi ya wafanya Biashara wa mifugo katika mnada wa Upili wa wilaya ya Igunga Mkoani Tabora Pamoja na kushukuru jitihada za Jeshi la Polisi katika kutoa Elimu kwa wafugaji wameomba elimu zaidi itolewe kwa wafugaji ili kujenga uelewa wa Pamoja.

Nae Meneja wa Mnada wa Upili Igunga Mkoani Tabora Bwana Yohana Mtende amesema hapo awali kulikuwepo na changamoto ya uzio wa kisasa katika mnada huo ambapo ameliomba Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo kuendelea kuimarisha Usalama wa Mifugo katika mnada huo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...