NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

WAZIRI wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt.Suleiman Jafo amewataka NEMC kuendelea kutoa elimu ya Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira kwa wananchi kwa Mujibu wa Sheria ili kuepukana na changamoto za kimazingira zinazojitokeza

Ameyasema hayo leo aliposhiriki kampeni ya soma na mti na kupanda miti takribani 500 katika Shule ya sekondari ya Dar es salaam girls iliyoko Luguruni Kata ya Kibamba, Manispaa ya Ubungo.

Amesema NEMC jukumu lao kubwa ni kuishauri Serikali namna bora ya Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira, hivyo kampeni ya soma na mti iliyolenga kutekeleza agizo la Serikali la kila Halmashauri kupanda miti milioni 1.5 ili kufikia lengo la kupanda miti takribani milioni 276 kwa mwaka kwa Halmashauri zote 184 nchi nzima ni jambo linalotakiwa kutiliwa mkazo na wataalamu wa Mazingira hasa NEMC.

Ameongeza kuwa upandaji wa miti utasaidia katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi zinazoweza kuleta athari kubwa.

" Tanzania ni wahanga wa athari za mabadilko ya Tabianchi, kunasehemu nyingine ukienda ukame umeshamiri, kwingine mvua zisizo na kipimo zinanyesha na kuleta athari kubwa, kwingine joto linaongezeka, yote haya ni athari za mabadiliko ya tabianchi yanayotokana na uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu, hivyo tuendelee kupanda miti na tuitunze" Amesema Jafo.

Pamoja na hayo mesema kila mtu anawajibu wa kupanda miti hivyo basi wameona ni vyema kushirikisha wanafunzi wote nchini kufanya zoezi hilo lidumu kuwa endelevu katika vizazi vyao.

Aidha Dkt,Jafo amewashukuru mawakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) kwa juhudi zao za kuzalisha miche ya miti kwa ajili ya kupanda nchini ili kuondokana na adha ya mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo yamepelekea kupungua kwa mvua na kuongezeka kwa kina Cha bahari.

"Tumeshuhudia dunia nzima joto linaongezeka ambapo joto hili linasababisha athari kubwa katika maisha ya wanadamu na viumbe mbalimbali lakini sehemu nyingine ukame umeshamiri,mvua ambazo hazina utaratibu zinasababisha mafuriko"Dkt,Jafo amesema

Amesema uharibifu wa mazingira umesababisha changamoto ya uchumi,umeme kukatika kutokana na ukosefu wa mvua za kutosha kwa ajili ya uzalishaji wa umeme,jambo ambalo limeibua upungufu wa uzalishaji nishati hiyo.

Pamoja na hayo ameeleza kuwa katika maelezo ya nchi na ilani ya chama cha mapinduzi imeagiza kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5 kwa mwaka kwa lengo la kupanda miti zaidi ya milioni 200 katika halmashauri zote ambapo katika taasisi za serikali wanafunzi kushiriki kufanya zoezi hilo.

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffar Nyaigesha ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa ya shule hiyo ya wasichana.

Kampeni hiyo ya upandaji miti imefadhiliwa na Benki ya NMB ambao wamekuwa wadau wakubwa wa Uhifadhi wa mazingira nchini,ambapo wanachama wa chama Tawala (CCM),Mabarozi wa mazingira,Pamoja na Mawakala wa huduma za misitu(TFS) wamehudhuria katika tukio hilo.


Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiongoza wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Dar es Salaam kupanda miti zaidi ya 450 katika utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akizungumza katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Jaffar Nyaigesha akizungumza katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati Waziri Jafo alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti ambayo inaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo ambapo ametembelea shule hiyo na kuongoza upandaji wa miti zaidi ya 450 leo Machi 15,2024.Baadhi ya walimu wa shule za sekondari katika halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakiwa katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti ambayo inaongozwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo ambapo ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana Dar es Salaam na kuongoza upandaji wa miti zaidi ya 450 kwenye shule hiyo leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akitoa cheti cha shukrani kwa baadhi ya wadau wa mazingira katika hafla ya utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti wakati alipotembelea katika shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa halmashauri ya manispaa ya Ubungo wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule za sekondari za halmashauri ya manispaa ya Ubungo wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti leo Machi 15,2024.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.Dkt. Suleiman Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam wakati wa utekelezaji wa kampeni ya Panda Mti katika shule hiyo leo Machi 15,2024.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...