Takdir Ali na Rahma Khamis. Maelezo. 27.03.2024.
WAAJIRI wa sekta binafsi nchini wametakiwa kuwaunganisha Wafanyakazi wao katika Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) ili waweze kupata matibabu na kutii matakwa ya Sheria.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Mbarouk Omar Mohammed wakati alipokuwa akifunguwa mafunzo kwa Waajiri wa sekta binafsi huko katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-wakili Kikwajuni Zanzibar.

Amesema afya ni nyenzo muhimu kwa Wafanyakazi hivyo ni muhimu kwa Waajiri wa sekta binafsi kuwaingiza katika Mfuko huo ili kupata matibabu wakati wanapopata matatizo.

Aidha amesema lengo la Mafunzo hayo ni kuwapa taarifa ya kuanza zoezi la usajili kwa Wafanyakazi wa sekta hiyo hivyo amewaomba Waajiri hao kuunga mkono zoezi hilo ili liweze kufanikiwa na kufikia lengo la Serikali la kutoa huduma za Afya kwa wote.

Hata hivyo amesema wamejipanga kuenda kuekeza zaidi huduma za Afya katika ngazi ya jamii kwani kunauhitaji mkubwa na kinga ni bora kuliko Tiba.

Kwa upande wake Mwanasheria wa ZHSF Thurea Gharib Mussa amesema kwa mujibu wa sheria ya ZHSF Waajiri wanatakiwa kujisajili na kuwasajili Wafanyakazi wao ndani ya siku 90 ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika.

Hata hivyo amewataka Wafanyakazi wa sekta binafsi kufanya haraka kujiunga ili ZHSF iweze kufanya usajili kwa makundi mengine na kuendesha zoezi hilo kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Nao Waajiri hao wa sekta binafsi Zanzibar wameomba kufanya haraka kuwaunganisha katika mfuko Wafanyakazi wao hususan Wazee kwani wamekuwa na matatizo mbalimbali yanayowakabili ikiwemo maradhi ya Presha na kuomba kushushwa katika ngazi za Wilaya ili kuwarahishia Wateja wao kupata huduma hizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) Mbarouk Omar Mohammed akifungua Warsha ya kuwajengea uelewa Waajiri wa sekta binafsi, juu ya kuanza kwa usajili wa Wafanyakazi wao katika Mfuko huo huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi Mfuko wa huduma za afya (ZHSF) Yassin Ameir Juma akizungumza na Wajiri wa sekta binafsi, iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Afisa Sheria kutoka Mfuko wa huduma za Afya (ZHSF) Thurea Gharib Mussa akiwasilisha sheria na dhana ya Afya kwa wote katika warsha ya kuwajengea uelewa waajiri wa sekta binafsi juu ya kuanza kwa usajili wa wafanyakazi wao katika mfuko huo huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Afisa tehama ZHSF Idrisa Makme Ukasha akiwasilisha mada ya usajili kwa wanachama katika warsha ya kuwajengea uelewa waajiri wa sekta binafsi juu ya kuanza Kwa usajili wa wafanyakazi wao katika mfuko huo huko Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.
Mwakilishi wa Jumuiya ya wastahafu na wazee Zanzibar Halima Tawakal Khayrallah akichangia katika warsha ya kuwajengea uelewa waajiri wa sekta binafsi juu ya kuanza Kwa usajili wa wafanyakazi wao katika mfuko huko katika Ukumbi wa Sheikh Idrissa Abdul-wakil Kikwajuni Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...