Na Mwamvua Mwinyi, Kisarawe April 4

Mkazi wa kijiji cha Vikumburu Wilayani Kisarawe ,mkoani Pwani, Daud Juma, amejeruhiwa na mapanga katika sehemu mbalimbali za tumbo lake na kikundi cha vijana walioambatana na Mwenyekiti wa kijiji hicho Ramadhan Chaka wakidai anaingilia wanawake kimapenzi kwa mtindo wa kishirikina (popobawa) .

Kutokana na Mwenyekiti huyo kushindwa kutumia nyadhifa yake kudhibiti kikundi hicho,!" Jeshi la Polisi limemkamata kwa ajili ya uchunguzi .
Kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk.  Fredy Shayo amethibitisha kupokelewa kwa  majeruhi huyo akitokea kituo cha afya Chole huku.

Hata hivyo alieleza, kutokana na hali ya majeruhi anaendelea kupatiwa matibabu.

Akielezea juu ya tukio hilo lilivyotokea majeruhi ambae amelazwa hospital ya wilaya ya Kisarawe , Daudi Juma amefafanua kwamba siku ya tukio alikuwa kwenye kibanda chake shambani na ndipo alitokea Mwenyekiti na kikundi cha vijana wengi wao wanafahamika.

"Nilipoona hivyo nilishika panga , Mwenyekiti akaniambia niweke panga chini na nikae chini ,akaniambia wewe unadaiwa ni mbakaji,nikashtuka na kusimama nikawaambia mimi sijawahi kubaka ghafla wakaanza kunipiga na mapanga tumboni, nikaanguka chini wakaondoka"

"Baadae nilipata nguvu nikakimbilia kwa jirani, nikachukua boda na kukimbizwa Chole hospital,laiti kama nisingeinuka kujinusuru nisingekuwepo hapa sahizi "alijieleza Daud.

Kwa upande wake mdogo wa majeruhi Baisi Masinga alibainisha, Mwenyekiti alikuwa na vijana zaidi ya kumi na kufanya msako wakimtafuta mtu anaedaiwa kuwa anakwenda kwa wanawake kisha anawatisha na kuwaingilia kimwili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani ,Pius Lutumo akizungumza kwa njia ya simu alikiri kutokea tukio hilo .

Alisema, wamepokea taarifa ya mtu mmoja kujeruhiwa, kulikuwa na uvumi kuwa mtu huyo mwanaume anapitia wenzake kwa mtindo wa popobawa yaani kwa imani za kishirikina.

Lutumo alifafanua,uvumi huo uliwaingia watu wachache wakaanza kumtafuta na walipompata wakamshambulia huku Mwenyekiti akiwepo pasipo kuzuia, kudhibiti wala kuchukua hatua yeyote hadi polisi walipoenda.

Kutokana na hilo, Jeshi la Polisi limemkamata Mwenyekiti huyo ili atoe ushirikiano kwa kosa la kushambuliwa kijana huyo .

Lutumo alitoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake wawe wanatoa taarifa kwenye vyombo vya kisheria kwa kwa hatua zaidi.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...