Benki ya Absa Tanzania imesema itaendelea kuweka kipaumbele katika kufanikisha ndoto za kielimu za watoto wa kitanzania katika kuboresha huduma za kibenki zinazohusu watoto, hususan akaunti yake maalumu ya watoto ya Absa Child Savings Account.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla waliyowaandalia watoto wenye uhitaji kutoka katika vituo vya watoto yatima vilivyo chini ya Taasisi ya Adonai El Roi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa, Bi. Ndabu Lilian Swere alisema hayo yanaenda kupitia lengo kuu la Benki Absa ambalo ni kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho Pamoja hatua Moja baadae ya nyingine kiuchumi sambamba na ahadi mpya ya Chapa yake isemayo ‘Tunathamini hadithi yako’.

“Watoto wana ndoto nyingi katika maisha yao, wapo wanaotamani kuwa madaktari, wanasheria, viongozi wa makampuni, viongozi wa kisiasa, tunathamini hadithi za watoto wetu, Absa tupo hapa kuwasapoti ili waweze kikamilisha ndoto za hadithi zao.

“Absa inatoa Huduma za kibenki kwa makundi mbalimbali, ni kwa kutumia huduma hizi pia tunawezesha hadithi za wazazi ama walezi wa watoto hawa nao pia kuweza kikamilisha hadithi zao mbalimbali za kiuchumi.

Hii si mara ya kwanza kwa Absa kufanya shughuli za kujitolea kusaidia jamii, hivi karibuni tulisaidia watoto wanaozaliwa kabla ya siku zao, hawa pia tutaangalia ni namna gani nyingine bora zaidi ya kuwasaidia”, aliongeza Bi Ndabu.

Akizungumza kuhusu akaunti ya watoto ya benki hiyo, Mkuu wa Mkakati na Bidhaa za Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Heristraton Genesis alisema akaunti hiyo haina makato ya mwezi na anaweza kupokea riba hata mara mbili endapo hatatoa pesa zaidi ya mara moja katika kipindi cha miezi mitatu.

“katika kuonyesha Benki ya Absa imejipanga vizuri katika kuziwezesha ndoto za watoto, tunatoa riba mara mbili katika kile kiasi kilichokaa ndani ya miezi mitatu Ili kuwarejeshea watoto waweze kukamilisha hadithi za ndoto zao za kielimu.

“Ni rahisi kufungua akaunti hii, mahitaji ni kitambulisho cha taifa cha mzazi ama mlezi, cheti cha kuzaliwa cha mtoto ama utambulisho wowote kutoka shule anakosoma mtoto, na akaunti inaweza kuendeshwa kwa kutumia huduma zetu za kidigitali bila kuhitajika kufika katika matawi ya benki”, alisema Bwana Genesis.

Naye Mwanzilishi wa asasi ya Adonai El Roi inayolea vituo mbalimbali vya watoto nchini, Bi. Ngole Melaisho alisema lengo lao kubwa la shirika lao lisilo la kiserikali pamoja na mambo mengine ni kutokomeza umasikini katika vituo hivi.

“Taasisi yetu Ina malengo ya kuwafuatilia watoto hawa kwa umakini waweze kuendeleza ndoto zao kwa kupitia kukuza vipaji vilivyo ndani yao.

“Nipende kuhamasisha watanzania waendelee kusaidia vituo hivi na pia kuongeza upendo kwa watoto hawa waweze kukamilisha malengo yao”, aliongeza Bi. Ngole.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...