Waziri wa Maji Mhe Jumaa Hamidu Aweso amesisitiza kazi ya utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bwawa la Kidunda kufanyika kwa staili isiokuwa ya kawaida ili kukamilika kwa wakati kwani mradi huu ni muhimu na wa Kimkakati.

Waziri wa Maji ameyasema hayo alipofanya kikao na Uongozi wa Ngazi ya Juu wa Kampuni ya Sinohydro Corporation ambao ndio watejelezaji wa Mradi huu akiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri na Sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Maji.

Mradi wa Maji wa Bwawa La Kidunda unaojengwa mkoani Morogoro una gharama Bil.329 ukizalisha lita Bilioni 190 na umefikia asilimia 20% kwa kazi ambapo kwasasa kazi ya usanifu na kazi ya ujenzi inaendele na unatarajiwa kukamilika mwezi June 2026.

Mradi huu wa Bwawa unajengwa lengo la msingi ni kuhakikusha kuwezesha uhakika wa uwepo wa Maji ya uhakika na kutosha katika mto Ruvu kwa kipindi cha Mwaka mzima ili kuwezesha na wanufaika kupata maji toshelevu wakati wote hata nyakati za ukame.

Sambamba na hilo Pia mradi huu utaweza kuzalisha umeme megawati 20, utahusisha ujenzi wa njia ya kusarisha umeme KM 101 mpaka kufika kituo cha kupoozea umeme cha Chalinze kuelekea kwenye gridi ya Taifa.
Aidha mradi huu utasaidia kilimo cha Umwagiliaji, ufugaji na Uvuvi pamoja na utunzaji wa Ikilojia ya Mto Ruvu.

Katika hatua nyingine Waziri Aweso amewapongeza kwa kazi nzuri waliofanya ya kujenga na kukamilisha kwa asilimia mia Mradi mkubwa wa Maji wa Kihistoria wa Jiji la Arusha uliogharimu kiasi cha Bilion 520 ambao upo katika hatua ya uangalizi kwasasa.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...