Na WAF, Dodoma

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa kuanza kwa utekelezaji wa bima ya Afya kwa wote itakuwa suluhu ya kudumu ya utekelezaji wa Sera ya wazee kupata matibabu bure katika kila Kituo cha Afya nchini.

Dkt. Mollel amebainisha hayo kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15 na kikao cha kwanza wakati akijibu swali Namba 12 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maakum Mhe. Tauhida Cassian Gallos aliyeuliza Je, kuna mkakati gani wa kuhakikisha Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika kila Kituo cha Afya nchini

“Wazee wasio na uwezo wa kugharamia huduma za Afya wameendelea kupatiwa huduma hizo kwa utaratibu wa msamaha hata hivyo ni kweli kuna changamoto kwenye baadhi ya maeneo”, ameeleza DKt. Mollel

Dkt. Mollel ametoa wito kwa wabunge na madiwani kuhakikisha wanashirikiana ili kusimamia Sera ya Wazee kupata matibabu bure inatekelezwa katika maeneo yao ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa sera hiyo katika maeneo yao.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...