BANKI of Africa Tanzania (BOA) ipo mbioni kuandaa Jukwaa la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara wa ndani ili kutoa fursa ya kuonyesha bidhaa na huduma zake katika juhudi za kukuza ushirikiano baina yake na wateja sambamba na kuchochea biashara na uchumi wa nchini kwa maendeleo ya taifa zima.

Akizungumza katika futari iliyoandaliwa kwa wateja wake mkoani Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Wasia Mushi, alisema kwamba lengo la kuandaa Jukwaa hilo la kibiashara na ni kuwaleta pamoja wafanyabiashara ili waweze kubadilishana uzoefu,


“lengo kuu la Jukwaa hilo ni wafanyabiashara kuongeza na kupanua wigo wa biashara zao na kuzileta pamoja na kuzionyesha na kufungua fursa ya biashara na kupanua wigo wa mahusiano na mitandao ya kibiashara,” alisema Bw Mushi

Alisema pia benki hiyo itaendelea kuandaa makongamano na mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuhusu mambo ya kodi , usimamizi wa fedha na huduma zingine za kibenki kuendelea kusogezwa karibu na wateja katika juhudi za kuwarahisisha wateja wao huduma za kibenki.

Bw Mushi aliongeza pia benki hiyo itaboresha na kuendelea kukuza huduma zake za kibenki ikiwamo huduma za uwakala , simu na mifumo yote ya matumizi ya teknolojia (Tehama) katika jitihada za kukuza biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchini.

“benki yetu inatoa ahadi kuendelea kutoa huduma bora na uwajibikaji wa hali juu katika kuhakikisha ustawi wa wateja wetu na kuchochea maendeleo uchumi katika sekta mbalimbali hapa nchini,” aliongeza Bw Mushi

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa ni heshima kwa uongozi wa Benki kuandaa Iftar kwa wateja wa benki hiyo, pamoja na kukuza hisia za jumuiya kati ya imani mbalimbali.

Alisisitiza zaidi umuhimu wa kushiriki pamoja kupata Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na umuhimu wa kuishi pamoja kidini na kuheshimiana kwa ajili ya kudumisha amani, maelewano na ustawi wa jamii.

Aliwathibitishia wateja wa benki hiyo kuhusu mkakati makini wa benki kuboresha huduma zake za kifedha kuendana na matakwa yao ikilenga zaidi kukuza makundi ya Biashara Ndogo na za Kati (SME) ambazo ni sehemu muhimu katika kuchangia ukuaji wa Pato la Taifa.

Pia alieleza ni kwa jinsi gani Benki imejipanga kuboresha huduma zake katika kuhudumia makundi yote ya wateja kuanzia wateja binafsi,Wafanyabiashara na makampuni katika kufanikisha ajendaza Serikali za kukuza ushirikishwaji wa kifedha nchini.

Kwa upande wake Sheikh Ramadhan Shareef Koba,kutoka Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) aliipongeza Bank of Africa Tanzania, kwa kuandaa Iftar, huku akigusia moja ya hadithi za Mtume Muhammad, kwamba “anayemlisha muumini aliyefunga hulipwa sawa na baraka zote za waliokaribishwa.”
Wateja na wageni walioalikwa wakiwa na Kaimu Mkurugenzi,Wasia Mushi
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa,Wasia Mushi akiongea na wateja walioalikwa kwenye Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo jijini Dar es Salaam
Sheikh Ramadhan Shareef Koba kutoka BAKWATA akitoa mawaida katika Iftar iliyoandaliwa na Bank of Africa





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...