Na Mwandishi wetu.

BANK of Africa Tanzania (BOA) imeeleza dhamira yake ya  kuimarisha huduma zake ili kuendana na matakwa  ya wateja sambamba na kuunga mkono jitihada za Serikali za kuwawezesha wanachi  kujipatia maendeleo sambamba na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.

Akiongea katika Iftar iliyoandaliwa na Benki hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Wasia Mushi, amesema benki hiyo itaboresha na kuendelea kukuza huduma zake za kibenki ikiwamo huduma za uwakala , simu na mifumo yote ya matumizi ya teknolojia (Tehama) katika jitihada za kukuza biashara na kuchochea ukuaji wa uchumi na kuwezesha makundi ya biashara ndogo na biashara za kati.

“benki yetu inatoa ahadi kuendelea kutoa huduma bora na uwajibikaji wa hali juu katika kuhakikisha ustawi wa wateja wetu na kuchochea maendeleo uchumi katika sekta mbalimbali hapa nchini,” ameongeza Mushi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa ni heshima kwa uongozi wa Benki kuandaa Iftar kwa wateja wa benki hiyo, pamoja na kukuza hisia za jumuiya kati ya imani mbalimbali.

Amesisitiza zaidi umuhimu wa kushiriki pamoja kupata Iftar katika mwezi mtukufu wa Ramadhani na umuhimu wa kuishi pamoja kidini na kuheshimiana kwa ajili ya kudumisha amani, maelewano na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein ameipongeza Benki ya Afrika Tanzania kwa kuandaa Iftar, na kwa jitihada inazofanya kushirikiana na Serikali katika kuwaletea Wananchi maendeleo.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji,Wasia Mushi akiongea katika Iftar hiyo ya wateja


Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Abdulgulam Hussein akizungumza wakati wa Iftar iliyoandaliwa na BOA bank kwa wateja wake wa ZanzibarMichuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...