Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango aliyoitoa kwaajili ya wakazi wa Wilaya hiyo hususani watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Tarehe 07 Aprili 2024.


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa sadaka ya futari kwa Wakazi wa Wilaya ya Mafia mkoani pwani hususani watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Mafia mara baada ya futari hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Bi. Aziza Mangosongo amemshukuru Makamu wa Rais kwa sadaka aliyotoa kwa watu wa Mafia na kuahidi kwamba wananchi wa Wilaya hiyo wataendelea kuwaombea heri na baraka viongozi wote.

Mkuu wa Wilaya amewasihi wananchi wa eneo hilo kuendelea kujitoa kwaajili ya wengine wakati huu wa mfungo Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo. Amewaasa wananchi wa Wilaya hiyo kutenda mema kama ambavyo mwezi Mtukufu wa Ramadhani unavyofunza pamoja na kuendelea kuchangia katika masuala muhimu kwaajili ya Mwenyezi Mungu ikiwemo katika nyumba za ibada.

Pamoja na sadaka ya futari pia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wamekabidhiwa vitendea kazi vya kusomea ikiwemo madaftari na kalamu kwaajili ya kuwasaidia mashuleni.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
07 Aprili 2024

Mafia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...