Na Janeth Raphael -MichuziTv -Dodoma

Serikali ya Tanzania na Uingereza zimesaini mkataba wa makubaliano wa ushirikiano wa miaka mitano wenye thamani ya Sh.Trilioni tatu unaolenga kukuza maendeleo katika sekta za afya, uwekezaji wa kijamii na ukuaji wa uchumi jumuishi.

Akizungumza katika hafla hiyo, leo Aprili 5,2024 jijini Dodoma Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof.Kitila Mkumbo, amesema katika mkataba huo eneo la kuchochea biashara na uwekezaji zitatolewa sh.Bilioni 300.

“Leo nimekutana na Waziri wa Uingereza wa Maendeleo na Afrika Andrew Mitchell, tumeshuhudia utiaji saini wa mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya ustawi kati ya Tanzania na Uingereza ambao umesainiwa kati ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dk.Tausi Kida na Balozi wa Uingereza nchini David Concar na katika maeneo haya ya biashara na uwekezaji tunatarajia zipatikane Paundi za Uingereza Milioni 100 sawa na Sh.Bilioni 300,”amesema Prof.Mkumbo

Aidha amesema kuwa katika mkataba huo Tanzania itashirikiana na Uingereza kufanya uwekezaji kwenye madini ya kimkakati, utajikita katika kuongeza thamani hapa hapa nchini.

“Lengo la Rais Samia Suluhu Hassan ambalo amelisukuma sana ni kuongeza thamani mazao yetu ya madini hususan madini ya kimkakati ambayo yanahitajika sana kwenye Green environment katika kutengeneza betri, kwa hiyo jambo hili tumelipokea vizuri kwasababu linalenga kwenda kutuongezea uwezo wetu sisi wenyewe,”amesisitiza

Wakati huohuo Waziri Prof. Kitila Mkumbo amekutana na ujumbe wa Serikali ya Denmark na kujadiliana juu masuala mbambali ikiwamo Biashara, Uwekezaji pamoja na mchakato wa uandaaji wa Dira mpya ya maendeleo ya Taifa ya miaka 25 ijayo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...