WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe Deogratius Ndejembi amekutana na Menejimenti na Watumishi wa Wizara hiyo katika Ofisi za Wizara Mtumba jijini Dodoma ikiwa ni siku yake ya kwanza akiwa kwenye nafasi hiyo tokea ateuliwe Machi 31, 2024 na kuapishwa April 04, 2024.

Katika kikao chake na Menejimenti na Watumishi wa Wizara amesisitiza umoja, ushirikiano na weledi katika kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi ili kufanikisha azma ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuwahudumia na kuwaletea maendeleo watanzania.

Mhe Ndejembi aliambatana na Katibu Mkuu Mpya wa Wizara hiyo, Mary Maganga na kupokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...