Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata akizungumza na wadau mbalimbali katika  hafla ya kufuturisha iliyofanyika leo April 5, 2024 katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.Na Karama Kenyunko Michuzi Tv
KAMISHNA Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata amewaagiza watumishi wa mamlaka kuzingatia maadili na kuonyesha kuwa kwa pamoja wanaweza kulipa kodi na kukusanya mapato ya Serikali kwa ufanisi na uaminifu ili kulijenga Taifa.

Pia amewataka watumishi hao kujitahidi kuwa wakweli na waadilifu katika kazi zao ili ziwe bora kwa wengine na wajitahidi kuwajibika ili kuleta matokeo chanya kwenye jamii.

Kamisha Kidata ametoa kauli hiyo katika hafla ya futari ya pamoja na watumishi na wadau wa mamlaka hiyo iliyofanyika Ijumaa Jioni ya Aprili 5, 2024 jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza kuwa TRA itaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu.

“Sisi, kama watumishi wa umma, pamoja na wadau wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, tuna jukumu la kuhakikisha kuwa tunalitumikia taifa letu kwa uaminifu na kwa kuzingatia maadili yetu ya kitanzania, sheria, kanuni, na taratibu za kazi zetu.

“Wakati huu wa funga ya Ramadhan, ni wakati mzuri wa kufanya tafakari juu ya matendo yetu ya kila siku kwa kuzingatia wajibu wetu wa kulipa kodi kama wananchi wenye uzalendo na nchi yetu, na jukumu letu la ukusanyaji wa Mapato ya Serikali kwa maendeleo ya taifa letu,” amesema.

Amesema kwa kuzingatia utukufu wa mwezi huu wa Ramadhani, ni vyema wakazidisha ibada, kuzingatia na kuimarisha umoja na mshikamano walionao, kuwasaidia kwa moyo wale wote wenye uhitaji, pamoja na kuzidisha huruma na upendo kwa kila mmoja.

Awali akitoa mawaidha, Sheikh Juma Dadi alisema katika kipindi hiki cha mfungo wanaelekezwa umuhimu wa kuzingatia maadili.

Amesema katika kipindi hiki kumekuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili katika pande mbalimbali kuanzia taasisi za serikali na watumishi.

“Kumekuwepo na. utovu wa maadili hasa baadhi ya watu katika sekta walipo. Kwa utovu wa maadili watu wamekuwa wakikosa haki katika kupata huduma za msingi badala yake watoa huduma wanataka rushwa. Wanafichaficha wanasema takrima.

“TRA pia wanalalamikiwa sana kutokana na utoaji huduma mara nyingi wananchi wanaambiwa hakuna mtandao wakati ni kwa makusudi lengo ni kuchelewesha watu ili kutengeneza mazingira ya rushwa. Wapo wachache wanaoharibu sifa ya taasisi mnayotumikia, hivyo ni lazima kuliangalia hili,’ alisema Sheikh Dadi ambaye alimuwakilisha Sheikh wa Wilaya ya Ilala Sheikh Adam Mwinyipingu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...