AKINA Mama katika wilaya ya Nzega mkoani Tabora wamenufaika na Elimu na huduma ya uzazi wa mpango kupitia mafunzo yaliyotolewa na shirika la Marie Stopes kwa watoa huduma na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kupitia mradi wake wa PSS(Public Sector Strengthen ).

Hayo yamesemwa na mtoa huduma ngazi ya jamii Amina Hamis ambaye alipatiwa mafunzo hayo na kuyafikisha kwa jamii husika ambayo imepokea elimu hiyo kwa kiwango kikubwa.

Amina alisema kuwa mafunzo toka Marie Stopes yamemsaidia kufikisha ujumbe kwa jamii hivyo kuokoa wakina mama wengi kutokana na changamoto za ukosefu wa limu na huduma za uzazi wa mpango. Kabla ya kuwapa elimu hiyo kina mama walikuwa wanazaa bila mpango hali iliyowapelekea kukosa muda wa kupumzika na kufanya mambo mengine ya kukuza uchumi.

“mwanzo kina mama walikuwa wana uzazi wa kuto kupangilia, walikuwa wanazaa mfululizo mwaka mtoto mwaka mimba lakini baada ya mimi kwenda mafunzo nilipoipata elimu hii na mimi nikaingia katika vitongoji, nilianza na kitongoji cha Ikena kuelimisha kina mama katika makundi ya kina mama ili kutoa elimu ya uzazi wa mpango” alisema Amina.

Pia aliongeza kuwa ametumia mafunzo hayo kupeleka elimu hio kwa vijana na wasichana ili kupunguza mimba za utotoni na zisizotarajiwa..

Kwa upande mwingine bi amina aliliomba shirika kumsaidia usafiri wa baiskeeli ili aweze kuwafikia wateja wengi zaidi kwani inamchukua mda mrefu kufika kitongoji kimoja kwenda kingine ili kuwafikia wakina mama kwa urahisi zaidi na kuwapa elimu hiyo.

Kwa upande wake muuguzi katika kituo cha afya cha Bukene Kulwa Charles Lesha alisema kuwa baada ya yeye kupata mafunzo ya uzazi wa mpango, yamesaidia kuongezeka kwa wateja kituoni hapo kutokana na wanawake wengi kuvutiwa na elimu hiyo.

Aliongeza kuwa kupitia mradi huu wa PSS ambao unalenga kuwezesha vituo vya serikali kwa kutoa mafunzo , vifaa na ufuatiliaji shiikishi wauguzi wamekuwa wakipata mafunzo ya mara kwa mara pamoja na kuongezewa vifaaa mbalimbali ikiwemo njia zote za uzazi wa mpango ambapo inawasaidia wateja kupata huduma zote katika kituo hicho bure.

Aidha ameishukuru Marie stopes kwa kuwawezesha wahudumu wa afya kupata elimu na kuwajengea uwezo watoa huduma, kuwezesha upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango.

Nao wanufaika wametoa ushuhuda kwa kunufaika na Elimu na huduma ya uzazi wa mpango, ambapo hapo nyuma kabla ya kupata elimu ya uzazi wa mpango walizaa mfululizo bila kupumzika.

“kwa jina naitwa Sijali Kulwa naishi msalala nina Watoto sita, familia yangu mimi mwenyewe imenufaika, mara ya kwanza nilikuwa nazaa tu, kila mwaka nina mimba hapo ndio nikaona usumbufu kwangu, kwa ukuaji wa mtoto n ahata kwa mume wangu nikaamua nitumie njia ya uzazi wa mpango ambapo nilianza na sindano”

Kwa upande wake mtoa huduma wa kiume ngazi ya jamii John Mtole alisema kuwa kwa upande wake anasisitiza ushiriki wa wanaume kwwenye masuala haya ya uzazi wa mpango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...