Na. Damian Kunambi, Njombe.

Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Ludewa mkoani Njombe zimesababisha maafa katika baadhi ya maeneo na hasa katika tarafa ya Masasi ambapo vijiji zaidi ya 6 vya tarafa hiyo vimeathiriwa baada ya maji kuingia ndani ya nyumba zao huku mawasiliano ya barabara yakikatika pamoja na mazao ya chakula kusombwa na maji mashabani.

Joseph Haule, Wilgis Mahundi na Grace Haule ni wakazi wa vijiji vya Liugai, Kiyogo na Kipingu vilivyokumbwa na maafa hayo wameiomba serikali iwasaidie chakula pamoja na sehemu za kukaa kwani mashamba yao yamesombwa na maji huku baadhi ya nyumba zikititia na nyinine kujaa maji.

Joseph Kamonga ni mbunge wa jimbo la Ludewa akiwa sambamba na katibu wa chama cha mapinduzi wilayani humo Gervas Ndaki wamefika katika vijiji hivyo na kujionea hali halisi.

Akizunguzumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kufika katika vijiji hivyo mbunge wa Jimbo hilo Joseph Kamonga ametoa pole kwa waathirika wa maafa hayo huku akitoa suluhisho la kudumu la mafuriko hayo kuwa ni mradi wa bwawa la kufua umeme na kilimo cha umwagiliaji wa Kikonge ili waweze kuyavuna maji hayo na kuyafanya kuwa fursa.

"Lile bwawa watakaloweka pale watapanda samaki wa aina mbalimbali liwe kama mtera, mtera wanazalisha umeme megawatt mia na kitu, lakini bwawa hili litazalisha umeme megawatt 300 na mradi huu utadhaminiwa na benki ya maendeleo ya Afrika, kwahiyo serikali yetu inaangalia suluhisho hilo". Amesema Kamonga

Aidha Kamonga ameongeza kuwa ataendelea kuihimiza serikali ili iweze kutoa msaada wa haraka ili waathirika waweze kupata msaada.

"Kwahiyo ndugu zangu mimi nipo pamoja na nyinyi, nitaendelea kuwasemea bungeni, kuwatetea kuhakikisha hizi changamoto zinatatuliwa".

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Gervas Ndaki amesema wao kama chama wameenda kuona ili waone namna ya kuhimiza serikali ili iweze kutimiza baadhi ya majukumu yake ikiwemo huo mradi wa umeme pamoja na umwagiliaji ambao utapunguza kasi ya maji kwenda kwenye makazi ya watu kwani hiyo ndiyo tiba halisi.

"Mimi nimshukuru Sana Mbunge wetu amekuwa anahimiza, tunayo miradi mingi sana Mheshimiwa Mbunge amekuwa akihimiza katika wilaya yetu ya Ludewa ikiwemo huu mradi wa umwagiliaji". Amesema ndaki

Ameongeza kwa kuwataka wananchi kuchukua tafadhali hasa za kiafya na kuwataka wananchi hao wasinywe maji bila kuchemsha kwani kipindi cha mafuriko kuna hatari ya kuibuka magonjwa ya milipuko hasa kipindupindu.

Naye Katibu Tarafa ya Masasi George Kapongo ametoa taarifa fupi ya mvua hizo na kusema mvua hizo zimenyesha maeneo ya milimani na kujaza mto Ruhuhu na Kipingu na kujaza maji kwenye mashamba ya watu. Pia amewataka wananchi kuepuka kupita katika maeneo yaliyojaa maji kwani kunaweza kuwa na hatari ya uwepo wa mamba.

Amesema kwa sasa tathmini inaendelea kufanyika juu ya wahanga wa mafuriko hayo ili kutambua idadi ya kaya zilizo athirika.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...