Raisa Said,Bumbuli

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba ameziagiza Jumuiya za Chama cha Mapinduzi katika Jimbo hilo kubuni miradi ya kiuchumi ya kata itakayosaidia kukuza kipato miongoni mwao na kuboresha maisha yao.

Makamba ambaye alikuwa akizungumza na wananchi na viongozi wa jimbo hilo , alisema kuna umuhimu wa jumuiya hizo za UVCCM, UWT na Wazazi kuwa na Miradi ya Kudumu ambapo ameahidi kutoa fedha za mtaji jumla ya Sh milioni 108 kwa ajili juanzisha miradi hiyo katika kata zote 18 zilizopo Halmashauri ya bumbuli

Kuna jumla ya kata18 katika Halmashuri ya Wilaya ya Bumbuli na kila kata itapata jumla ya milioni 6 ambazo zitagawanywa kwa jumuiya tatu kwa ajili ya kuanzisha miradi hiyo nakwamba kila Jumuiya kwa kila kata ataipatia sh million 2

“Leteni maandiko yenu, halafu tutayaangalia kwa pamoja kabla ya kutoa mtaji. Nitatoa sh million 6 kwa kila kata kwa ajili ya miradi ya kuanzia kwa jumuiya hizi tatu kila kata ambazo sh milioni 2 kwa kila jumuiya,” alisema. Nakuongeza kuwa kwa wale wenye miradi watakuwa wanaongezewa na wale ambao hawana wanatakiwa kuandika maandiko.

Hata hivyo, alionya kuwa miradi hiyo isiwe ya kuwanufaisha vongozi bali iwe ya kusaidia watu wote wa Jumuiya hizo. Makamba alitoa mfano wa mradi wa mashine ya kutotolea ambayo alisema bei yake kama sh milioni 2.8.

Makamba alitoa ahadi hiyo baada ya kuombwa na viongozi wa Jumuiya hizo kuwasaidia ili waweze kijiinua kiuchumi, huko nyumba Makamba aliwahi kutoa fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya kanga na vitenge kwa ajili ya Jumuiya ya Wanawake. Mbunge huyo alitoa vitenge 35 kwa kila kata.

Akizungumza katika mkutano huo Hamis Abdalah Shekiogha, ambaye ni Katibu wa CCM Kata ya Vuga alimwomba Waziri kusaidia Jumuiya ya Wazazi nayo kuwa na miradi yao ili waweze kuisaidia kuboresha maisha. Alisema kuwa jumuiya hiyo imesahauliwa ilhali wao ni walezi wa Jumuiya zote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...