KAMPUNI ya Barrick nchini imedhamini kongamano la Vyuo vya elimu ya juu mkoani Mwanza lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania na kufanyika katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino ambapo wanafunzi walioshiriki walipata fursa ya kujengewa uwezo kuhusiana na masuala ya kujiamini,jinsi ya kujiajiri na kupata ajira sambamba na kutambua fursa zilizopo zinatozotokana na mabadiliko ya kidigitali yanayoendelea kutokea duniani.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino,Utawala na Fedha Prof Agnes Nyomola akiongea katika kongamano hilo.
.Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick walishiriki katika kongamano hilo
Afisa Rasilimali watu Mwandamizi Barrick, Renatus Malawa akimkabidhi zawadi za Tshirt Naibu Makamu Mkuu wa chuo cha cha Mtakatifu Augustino,Utawala na Fedha Prof Agnes Nyomola.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Chuo,AIESEC na wafanyakazi wa Barrick
Wanafunzi wakisiliza mada mbalimbali wakati wa kongamano hilo
Afisa Rasilimali watu Mwandamizi wa Barrick, Renatus Malawa, akiongea na wanafunzi katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Mtakatifu Augustino cha jijini Mwanza, wakionesha vipeperushi vya Kampuni ya Barrick vyenye QR codes wanazoweza kuskani na kupata fursa mbalimbali zinazotolewa na kampuni hiyo, wakati wa kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...