Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza na Wataalam kutoka Oxford Policy Management Ofisini kwake tarehe 09 Mei, 2024 Jijini Dodoma.
Mratibu wa Programu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bi. Adela Mpina (Kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao cha Wataalam kutoka Oxford Policy Management, Kushoto ni Mkururgenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Watoto kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tarehe 09 Mei, 2024 Jijini Dodoma.

Mshauri Elekezi kutoka Oxford Policy Management (OPM) Dkt. Emmanuel Maliti akieleza jambo katika kikao na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi walipomtembelea Ofisini kwake tarehe 09 Mei , 2024 Jijini Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU

Na Mwandishi wetu- Dodoma
KATIBU  Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi amekutana na kufanya mazungumzo na Wataalam kutoka Oxford Policy Management kuhusu Uwezekano wa matumizi ya akili bandia (Artificial Intelligence and Machine Learning) katika kufanya mapitio ya matumizi ya umma (Public Expenditure Review).

Kikao hicho kimefanyika tarehe 09 Mei 2024 ofisini kwake Jijini Dodoma ambapo Dkt. Yonazi amesema pia lengo la kikao hicho ni kujadili kuhusu makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (ECD) nchini Tanzania.

Ikumbukwe Serikali ya Tanzania ilizindua Programu ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali yam Mtoto (PJT-MMMAM) mwaka 2021 kama mpango mkuu wa kuzileta pamoja Wizara na wadau mbalimbali ili kuboresha Makuzi na maendeleo ya awali ya Watoto kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka 8.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...