Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza, leo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja 'Smart (kushoto mbele mwenye miwani),wa tatu ni Mjumbe wa NEC, Jamal Abdul 'Babu; na wa Pili kutoka kjulia ni Mkuu wa Wilaya, Hassan Masalla.


NA BALTAZAR MASHAKA,ILEMELA
KAMATI ya Siasa ya CCM, mkoani Mwanza,imevutiwa na ujenzi wa miundombinu ya shule mpya ya Kisenga,bweni la wasichana wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Buswelu,wodi ya wazazi ya Kituo cha Afya Buzuruga na barabara ya Buswelu-Mhonze yenye urefu wa kilometa 17.7.

Miradi hiyo inayogharimu sh.bilioni 3.5 inatekelezwa katika Manispaa ya Ilemela ikilenga kuboresha elimu,afya na miundombinu ya barabara ili kuifungua kiuchumi Wilaya ya Ilemela.

Akizungumza baada ya Kamati ya Siasa ya Mkoa kukagua miradi hiyo leo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ‘Smart’ amesema wanampongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa maono na kuelekeza fedha sh. milioni 584.2 kujenga shule mpya ya Kisenga Sekondari.

“Tunaelewa Rais Dk.Samia ana dhamira njema ya na sekta ya elimu na kuipa kipaumbele kikubwa, lakini pia fedha hizo zisingepata usimamizi mzuri tusingeyaona matokeo haya tunayoyashudia,”amesema Smart.

Ameeleza,miradi si tu inaridhisha bali imejengwa kwa ubora kwa kuzingatia thamani ya fedha, amemshukuru Rais Samia kwa fedha nyingi za miradi ya maendeleo alizoleta Ilemela katika sekta mbalimbali.

Hivyo dunia ya sasa kutokana na kuongozwa na Sayansi na Teknolojia, Smart ameiagiza serikali itafute njia ya kupeleka walimu wa masomo hayo ili kuwaondolea changamoto wanafunzi wa shule hiyo ya Kisenga.

Awali Mkuu wa shule hiyo,Getrude Ntemi,amesema baadhi ya miundombinu iliyojengwa kupitia Mradi wa SEQUIP ni vyumba viwili vya madarasa,jengo la utawala,maabara za Kemia na Baiolojia,Fuzikia,maktaba,kichomea taka na matundu ya vyoo imejengwa kwa sh.milioni 584.2 za mradi wa SEQUIP.

“Mradi umekamilika na unalenga kupunguza msongamano wa wanafunzi Kiseke sekondari lakini shule haina walimu wa masomo ya sayansi na TEHAMA,”amesema Ntemi na kumshukuru Rais Dk.Samia kwa maono, dhamira na kasi ya kuboresha elimu ili kuwezesha watoto kujifunza na kupambana na adui ujinga.

Aidha Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF),Leonard Robert amesema mradi wa bweni la wasichama 80 wenye mahitaji maalum wa Shule ya Msingi Buswelu,unajengwa kwa sh.milioni 164.3 uwawezeshe kupata mazingira rafiki ya kujisomea.

Amesema mradi huo unatekelezwa na mitaa miwili ya Bulola A kwa gharama ya sh.milioni 87.1 na Bulola B sh.milioni 77.2,unatarajiwa ukamilike Juni 30, mwaka huu kwa mujibu wa mkataba,lakini changamoto ya mfumo kutoruhusu malipo umechelewesha utekelezaji.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Mipango (TANROADS),Mhandisi Magesa Mwita,barabara ya Buswelu hadi Mhonze,urefu wa kilometa 17.7 inayojengwa kwa awamu na mkandarasi Mumangi Construction kwa gharama ya sh. bilioni 2.562 kwa kiwango cha lami, imefikia asilimia 75.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza,Smart amesema barabara hiyo imejengwa kwa ubora na thamani ya fedha inaoneka na kumpongeza mkandarasi kwa kazi nzuri huku akimhimiza aikamilishe kwa wakati.

“Kazi ya ukaguzi wa miradi ni ya kikatiba,CCM tuliahidi kuleta maendeleo yakiwemo ya barabara baada ya kuaminiwa na wananchi kwa ubora wa ilani yetu tukaunda serikali,hivyo tumekuja kukagua kuona mradi huu unavyotekelezwa na serikali,tumeridhishwa na kazi hii na tunampongeza mkandarasi pamoja na TANROADS kwa usimamizi,”amesema.
Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza, Kisenga Sekondari, leo wakiimba wimbo 'Hongera Mama Samia, oneni kazi nzuri ya uongozi wa Mama .Hongera Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mwanza, Akiwaongoza wajumbe ya kamati hiyo baada ya kukagua wodi ya wazazi kituo cha Afya Buzuruga, leo wilayani Ilemela.Kushoto ni Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Michael Masanja ;Smart', leo akizungumza na wananchi wa Buswelu, baada ya kamati ya siasa kukagua bweni la wasichana wenye mahitaji maalum llinalojengwa kwa ufadhili wa TASAF katika Shule ya Msingi Buswelu. Picha zote na Baltazar Mashaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...