Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Wakurugenzi kutoka Halmashauri zote za Jiji la Dodoma wametakiwa kuichukua fursa ya Mradi wa Accelerated Innovation Delivery Initiative-Livestock (AIDI-L) uliozinduliwa leo Jiji hapa na Mkuu wa Mkoa Mhe Rosemary Senyamule ambao umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Watu wa Marekani (USAID) kwa kwenda kuunda vikundi au kuwahamasisha wanawake na vijana katika maeneo yao ya kazi kwani mradi huu unalenga makurdi ya kimkakati ya wanawake na vijana.

Mhe Senyamule amesema hayo mapema Leo hii May 14,2024 katika Uzinduzi wa Mradi huo wa AIDI-L uliojikita zaidi katika sekta ya ufugaji wa kuku huku ukihudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta hiyo kutoka ndani na nje ya Nchi.

Na ameongeza katika sekta hii ya ufugaji wa kuku kuna suala ajira,uchumi na hata lishe hivyo kuna vitu vingi sana.

"Nimefurahi kuona Wakurugenzi mko hapa,Nawaomba mchukue hiu kama fursa muhimu sana kwa kwenda kuunda vikundi au kuhamasisha hao wanawake na vijana watumie fursa hii na mradi unapokwenda kuisha basi tuone thamani na kiasi gani wametuvusha kwenye uchumi kwa wanachi wale wenye vigezo vyote,ukiangalia hapa kuna lishe,kuna uchumi na kuna ajira pia kwahiyo tuna vitu vingi sana,mkiweka mipango vizuri tutapata kujua ni namna gani tumevuka kwenye lishe,uchumi na ajira".

Aidha Mhe Senyamule amesema kuwa Mradi huu utasaidia vijana wengi hapa Dodoma kupata ajira kwani hapa kuna vijana wengi vijana wengi wanaohitimu masomo yao katika vyuo mbalimbali vilivyopo hapa Dodoma wakati wakisubiri ajira au kujiajiri wenyewe na.mwisho wa siku kuweza kupanda kwa uchumi.

"Mradi huu utasaidia vijana wetu kupata ajira lakini mwisho wa siku uchumi wetu unategemea kilimo hata mapato ya halmashauri nyingi yanaongezwa na kilimo tulikuwa tunaangali GDP ndo inachangia kwa kiasi kikubwa ,lakini kilimo au ufugaji wenyewe ukilega mchango wake unakuwa ni mdogo".

"Sasa hiki mnachoenda kukifanya nyie itafanya pia tija katika huo uchumi itakuwa imeongezeka maana mnasema ni haraka na ubora na huenda ikiwa sio kubwa zaidi".

Naye Mratibu wa shuguli za Utafiti kwenye Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa mifugo hapa Tanzania Bwana Adolph Jeremiah ameeleza malengo ya mradi ambapo amesema mradi huu umelenga kutatua changamoto za kijinsia na kuwalenga hasa wanawake na vijana ambapo moja ya changamoto ni upatikanaji wa mbegu au mbali sahihi za mifugo hasa kwa wafugaji wa vijijini.

Na kuongea kuwa yapo malengo matatu mahsususi katika mradi huu ambayo ni pamoja na kuhamasisha na upatikanaji wa mbali sahihi,upatikanaji wa mitaji na kuhamasisha wafugaji kufaga kuku waliochanjwa na kupata huduma bora za ugani.

"Huu ni mradi ambao unalenga kutatua changamoto za kijinsia na tunawalenga hasa wakina Mama na vijana, changamoto ni upatikanaji wa mbegu au mbali sahihi za mifugo hususan kuku kwa wafugaji wa vijijini hasa wakina Mama na vijana na kuku ni mfugo ambao unafugika kwa muda mfupi na unaweza ukaonesha matunda kwa wafugaji kwa muda mfupi ndi maana ikawa ni kupitia mradi huu. Vijana wengi na akina mama hawana rasilimali kama ardhi na mitaji za kuwawezesha kuanzisha miradi mikubwa lakini kupitia kuku mitaji kidogo wanayotumia na kumletea tuja katika kipato chake".

"Malengo mahsusi yaliyopo kwenye mradi ni pamoja na kuhamasisha upatikanaji wa mbali sahihi ziliboreshwa hapa Tanzania kwa kuku wa nyama,kuku chotara na kuku wa mayai kulingana na mahitaji ya wafugaji na wale wanaostahimili mazingira kwa mijini na vijijini,kupitia mradi huu watapata kuku bora kabisa wale wa F1. Pili upatikanaji wa mitaji kwa wale wanaoanza na wale wanaotanua ufugaji wao mradi utahasisha Taasisi za kifedha ikiwemo EFTA kusaidia hili. Tatu kuhamasisha wafugaji wafuge kuku ambao wameshachanjwa na wapate huduma bora za ugani,matibabu na kuunganishwa na masoko".

Bwana Amos Omore wa Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Mifugo yeye ameeleza kuwa kwa nchi zingine sekta ya mifugo inachangia kwa kiasi kikubwa katika pato la Taifa lakini kwa hapa bado haijaweza kufanikiwa hivyo ni wakati sasa kupitia mradi huu kuona gani sekta ya mifugo inainuka na kuweza kuchangia pato la Taifa kwa uzuri.

"Ukiangalia sekta ya mifugo inachangia kwa kiasi kikubwa kwenye nchi zingine pato la Taifa lakini hapa haijaweza kufanikiwa kwa uzuri kwahiyo ni wakati sasa kuona ni namna gani kwa kupitia mradi huu tunaweza kuhakikisha tunainua sekta ya mifugo ili iweze kuchangia vizuri kwenye pato la Taifa na sisi kama ILRI tunaona kuwa sekta ya kuku pamoja na maziwa ndio eneo hasa ambalo linaweza kuleta chachu kwenye sekta ya mifugo ".

Naye Bi Neema Mrema kutoka Taasisi ya Venture37 amesema kuwa mradi huu wanategemea kumuinua Mama kwa kuhudumia familia yake kuwezesha lishe kuimarika.

"Mradi huu tunategemea kumuinua Mama na kuhakikisha Mama huyu anaweza kuhudumia familia yake na lishe nyumbani inaweza kuimarika".

Mradi huu utatekelezwa kwa miaka 2 ambapo utagharimu kiasi cha milioni kwa fedha za kimarekani na unalenga kuwafikia watu elfu 18000 kwa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...