Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limezindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia katika Mkoa wa Morogoro kwajili ya kuvitambua vikundi vya kinamama na makundi mengine ili shughuli zao za kijairimali ziweze kunufaika na program hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Adam Malima alisema hayo wakati wa uzinduzi wa program  hiyo ambayo umefanywa na NEEC kuwa uzinduzi huo ni hatua muhimu kwa mkoa wake katika kufanya watanzania kufanya shughuli za ujasiriamali kwa tija.

"Mkoa wetu umepokea mradi huu wa Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa mikono miwili,‘ na tunaahidi kufanya vizuri zaidi "alisisitiza

Alisema ili kumkwamua mwanamke ni lazima kumpatia uwezeshaji wa mafunzo na uwezeshaji na program hii imeanza kufanya hiyo na matokeo yake yatakuwa makubwa.

Alifafanua kwamba mkoa wao utatekeleza program ya Imarisha Uchumi ana Mama Samia kwa vitendo, na hiyo itasaidia kuwawezesha watanzania kufanya shughuli za uzalishaji.

Alisema Mkoa wa Morogoro kipaumbele chake kikubwa ni kilimo na wamejipanga kuingiza mbegu za karafuu, michikichi, cocoa na parachichi ambazo watagawa bure mbegu kama njia ya kuyawezesha makundi hayo kuzalisha na kupata utajiri

Alisema shughuli za uzalishaji mazao hayo ya kilimo na shughuli mbalimbali za kijasiriamali zitasaidia watanzania kujikwamua kivipato.

Katibu Mtendaji wa NEEC,Bi. Beng`i Issa alisema Program ya Mama Samia inalenga kuwakwamua akinamama kupitia vikundi vyao na makundi mengine ya watanzania likiwemo la vijana na wenye ulemavu.

Mkoa huu unafursa kubwa katika kilimo kutokana na ardhi nzuri yenye rutuba na watu wake wengi wanashughulisha na kilimo na shughuli nyingine za kijasiriamali baraza litatambua shughuli zao wanazofanya katika maeneoyao ili ziweze kupata uwezeshaji alisema.

Bi. Issa alifafanua kwamba baraza lake linawaratibu katika mikoa ambapo wanatumika katika kufanyakazi ya kusaidia makundi hayo kuingia katika kanzidata zao ili hatimaye waweze kunufaika na uwezeshaji utakaotolewa na program hiyo.

Aliendelea kusema program hiyo imekuja kuboresha shughuli zao za kilimo na shughuli zote za kijasiriamali wanazofanya na lengo ni kuwawezesha watanzania kuwa na maisha bora.

Pia aliwataka akinamama katika shughuli zao za kijasirimalia kukumbuka kuweka akiba katika benki au katika vibubu ili iwasaidie kupanua biashara zao.

Katibu wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mvomero,Bi. Sebastinana Mbaga alisema ujio wa program hiyo ni moja ya hatu ya kuwamua wanawake na makundi mengine kiuchumi.

Alisema katika wilaya yao wanafanya shughuli mbalimbali za kiuchumi za kijasiriamali za kilimo, kuongeza thamani mazao ya kilimo, uchuuzi na ujasiriamali mbalimbali.

Katika uzinduzi huo baraza likuwa pamoja na taasisi za kifedha ambazo zilitoa elimu namna umuhimu wa kufungua akaunti na kuweka akiba.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Beng"I Issa  akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Morogoro kuhusiana Program  ya Imarisha Uchumi na Mama Samia na kushoto kwake Ni Katibu Tawala wa Mkoa huo, Dkt.. Mussa Ally Mussa. picha na Mwandishi wetu Morogoro.
 

 Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi. Beng'i Issa akizungumza na makundi ya Kinamama wa Mkoa wa Morogoro wakati wa uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia kwa mkoa huo.
 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Adam Malima akizungumza na makundi ya kinamama wakati wa uzinduzi wa Program ya Imarika Kiuchumi na Mama Samia katika Mkoa wake, programa hiyo inatekelezwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa makundi ya kinamama na makundi mengine.
 

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Adam Malima katikati akifuatilia maelezo kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi NEEC. B. Beng'i Issa (kusho)kuhusu program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia, ambayo ilizinduliwa Mkoani humo. wengine viongozi na watumishi mbalimbali wa Mkoa huo Mkoani humo.
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi NEEC, Bi. Beng'i Issa katikati akiwa na makundi ya Kinamama wakati wa Uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia wakati wa uzinduzi wa Program hiyo kwa Mkoa was Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...