Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA), Neli Msuya ametembelea Kata ya Lwanhima kwa lengo la kukagua hali ya upatikanaji wa huduma baaada ya miundombinu ya maji inayopeleka huduma katika Kata hiyo kuathiriwa na ujenzi wa barabara ya Igoma- Buhongwa.

Neli amefanya ziara hiyo Mei 21, 2024 akiwa ameambatana na Diwani wa Kata ya Lwanhima, Marko Swalala pamoja na Timu ya wataalam kutoka MWAUWASA.

"Nimefika hapa kukagua hali ya huduma ya maji lakini pia kuzungumza na viongozi katika Kata hii ya Lwanhima kuhusiana na hali ya upatikanaji wa huduma pamoja na jitihada na mipango inayoendelea kutekelezwa na Mamlaka," amefafanua Neli

Mkurugenzi Neli alifafanua jitihada za muda mfupi za muda wa kati na za kudumu zinazotekelezwa na Mamlaka katika kuboresha huduma ya maji kwenye maeneo yanayohudumiwa na MWAUWASA.

Alibainisha kuwa mtandao wa usambazaji maji katika Kata ya Lwanhima na kata zingine katika ukanda huo unaendelea kuboreshwa ili kuwezesha wananchi kunufaika na mradi wa Butimba.

"Katika hatua za muda mfupi, Mamlaka inalaza mabomba ya usambazaji maji kwa awamu katika mitaa hasa yenye changamoto ili kuboresha mfumo wa usambazaji," amesema.

Kwa upande wake Diwani Swalala alipongeza ujio wa Mkurugenzi Neli katika kata hiyo na kueleza kuwa amekuwa akishirikishwa kuhusu mipango inayohusu miradi ya maji.

"Tunakushukuru kwa ujio wako hapa, hii inaonyesha dhamira ya kipekee ya kulipatia ufumbuzi suala la changamoto ya maji katika kata yetu, huu ndio utumishi wa umma. Tunakushukuru, hakikia unatupa ushirikiano siku zote," amepongeza Swalala.

Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Neli alitembelea na kukagua miundombinu ya kusafirisha maji iliyoathiriwa sambamba na kuzungukia mtandao mzima unaotumika kusambaza maji eneo la Kata ya Lwanhima na tenki la Sahwa ya Juu ikiwa ni utaratibu aliyojiwekea wa kukagua hali ya upatikanaji wa huduma katika maeneo yanayohudumiwa na MWAUWASA
Kaimu Mkurugenzi wa MWAUWASA, Neli Msuya alipotembelea kukagua hali ya huduma ya maji Nyamagana, Mwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...