Na. Vero Ignatus Arusha
Shirika la Teenagers Talk Organization linalo jihusisha katika kusaidia watoto na vijana katika jamii kwa kutoa elimu ya kujitambua, huduma za afya za mabadiliko ya tabia na msaada wa kijamii huku Dhamira ya shirika hilo ikiwa ni kulinda jamii ambapo vijana wanaweza kufanikiwa, wakiwa na maarifa na rasilimali za kuendesha ukuaji na mabadiliko yao kwa kujiamini.
Wakifanya uzinduzi wa shirika hilo jiji Arusha Mkurugenzi wa shirika laTeenagers Talk organization Doricas Mgoya ameeleza kuwa wamekuwa wakitoa elimu kwa watoto, ili kuwasaidia watoto kuwa na ufahamu na kuondokana na changamoto za kimaadili, kimalezi na kiafya.
Aidha ameeleza kuwa wameweza kufikia watoto zaidi ya 2000 katika shule mbalimbali, makanisa na vituo mbalimbali Katika kuwapatia elimu. Huku akieleza kuwa malengo yao kwa mwaka 2024 hadi 2028 ni kuwafikia vijana wengi zaidi kupata elimu.
"Licha ya kutoa elimu baada ya uzinduzi huu tunatarajia kuanzisha karakana kubwa kwaajili ya kuwasaidia vijana wa kiume na wakike ili waweze kuwa na ushindani katika soko la ajira, pamoja na kutoa elimu kwa njia ya machapisho na vitabu bila gharama.
Kwa upande wake Zefhania Umburi ambaye ni miongoni mwa wazazi ambao watoto wao wanapatiwa elimu katika shirika hilo ameeleza kuwa shirika hilo linapaswa kutiwa nguvu kubwa ili kuwasaidia watoto na vijana kukuwa na kuishi maisha bora
Aidha ameongeza kuwa wamehimizwa juu ya malezi na makuzi ya watoto wao huku wakitakiwa kuzungumza na vijana wao ili waweze kuiga mambo mazuri kutoka kwa wazazi na walezi.
Nae Padri Denisi Ngowi ambaye ni mratibu wa idara ya usalama wa mtoto jimbo kuu Katoliki Arusha ameeleza kuwa vijana wengi wamekuwa wakiathirika na ukatili wa mtandaoni hivyo ni vyema watoto na vijana kuwa na umakini
" tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 60% ya vijana na watoto wanatumia mitandao ya kijamii na 4%tayari wamekwisha adhiriwa na kundi hili linazidi kukua kwa kuwa teknolojia nayo inazidi kukua"
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa shirika hilo Mhe Mathias Haule ambae ni Mkurugenzi wizara ya maendeleo ya jamii Aki muwakilisha katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii wanawake na makundi maalumu ameeleza kuwa mashirika hayo yamekuwa msaada mkubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo afya, elimu, mazingira, maji na maeneo mengine mtambuka
Aidha ameongeza kuwa kwa uzinduzi huu inaongeza wigo mpana wa kupanua uelewa wa jamii kwani kwa mujibu wa takwimu vitendo vya ukatili vilivyo ripotiwa tangu Januari hadi Desemba jumla ya matukio elfu kumi na tano mia moja hamsini na sita wasichana wakiwa 11987 wavulana 3159. Vitendo hivyo vikiwa ni pamoja na ubakaji, ulawiti, pamoja na mimba za utotoni.
'' takwimu hizi zimeshuka na hii ni kutokana na elimu zitolewazo na mashirika mbalimbali hivyo nayapongeza mashirika binafsi na niombe kwa kuwa serikali inafanya uzinduzi wa mpango wa kutokomeza ukatili kwa watoto katika kuboresha mpango huo"
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...