MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Jaji Mshibe Ali Bakari ametoa rai kwa wataalamu kutoka nchi za Kanda ya Afrika Mashariki kuboresha ushirikiano ili kuweza kukabiliana na changamoto zinazojitokeza hususani kipindi cha matukio ya hali mbaya ya hewa. 

 Mshibe alisema hayo wakati akifungua Mkutano wa Kamati ya Usimamizi wa Programu ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ya Utabiri wa Hali Mbaya ya Hewa kwa nchi Wanachama Kanda ya Afrika Mashariki, unaofanyika Dar es Salaam, kuanzia Mei 14-17, 2024. 

Aidha, alisisitiza kuwa, mkutano huo umewaleta pamoja wataalamu kutoka nchi za Tanzania, Burundi, Djibouti, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan, Uganda, Djibouti, Somalia, Eritrea, Sudan Kusini pamoja na Wataalamu wengine kutoka vituo mbalimbali vya Kikanda vya WMO, hivyo kupitia ushirikiano huo huduma za hali ya hewa kwa nchi wanachama wa WMO Kanda ya Afrika Mashariki zinatarajiwa kuboresha huduma zake  ili kupunguza athari zitokanazo na matukio ya hali mbaya ya hewa.

Akimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Kaimu Mkurugenzi wa TMA ofisi ya Zanzibar,  Masoud Faki alisema kupitia programu hiyo ya Utabiri wa Hali Mbaya ya Hewa, TMA imeweza kunufaika na masuala mbalimbali yakiwemo ya mafunzo kwa wataalamu na miongozo ya pamoja ya utendaji kazi ambayo imesaidia katika maandalizi ya utabiri katika ngazi ya nchi.

Masoud aliendelea kueleza kuwa mwaka 2019 Tanzania kupitia TMA ilichaguliwa na WMO kuendesha Kituo cha Kanda cha kutoa mwongozo wa utabiri wa hali mbaya ya hewa kwa nchi zilizopo katika Ukanda wa Ziwa Victoria ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. 

Katika hatua nyingine, mwakilishi kutoka sekretarieti ya WMO aliishukuru Serikali ya Tanzania kukubali kuandaa na kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu wenye lengo la kuboresha huduma za taarifa za hali mbaya ya hewa kwa nchi wanachama wa Kanda ya Mashariki, lengo ambalo linaenda sambamba na jitihada za Umoja wa Kimataifa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...