Mheshimiwa Dk Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, alipowasili katika Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar Es Salaam, kwa ajili ya uzinduzi wa albamu mpya ya Msanii wa Mziki wa Bongofleva, Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize au Konde Boy, uliofanyika ukumbini hapo, ukipewa kauli mbiu ya #MzikiwaMama, #SamiaDay, ambapo Rais Samia alikuwa mgeni rasmi. Wengine pichani ni pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Dk Damas Ndumbaro, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mhe. Albert Chalamila na Harmonize, ambaye pia ni Mmiliki wa Kundi la Muziki la Konde Music Worldwide.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Msanii wa Bongo Flavour Rajab Abdul aka Harmonize mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mlimani City kwa ajili ya kushuhudia uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mama Mzazi wa Msanii wa Bongo Flavour Harmonize, Habiba Baisa Chivalavala wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa Albamu ya Muziki wa Mama kutoka kwa Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 25 Mei, 2024.
Msanii wa Kizazi Kipya Rajab Abdul aka Harmonize akitumbuiza katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Albamu yake ya Muziki wa Mama tarehe 25 Mei, 2024. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...