Peter Haule, WF, Dodoma

Serikali imesema kuwa imeunda kamati ya kukusanya na kuchambua maoni na mapendekezo ya viwango vya nyongeza ya pensheni ili kuwezesha maandalizi ya rasimu ya Waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu nyongeza ya pensheni kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina.

Hayo yameelezwa bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta Mbogo, aliyetaka kufahamu lini Serikali itawaongezea pesheni wastaafu wanaolipwa shilingi 100,000 kwa mwezi na Hazina.

Alisema kuwa Kazi ya uchambuzi wa maoni na mapendekezo ya wadau kuhusu mapendekezo ya viwango vya nyongeza ya pensheni inatarajiwa kukamilika kabla ya tarehe 30 June 2024.

Aidha kuhusu fomula ya kikokotoo, Dkt. Nchemba alisema kuwa Kamati imeundwa na inahusisha watu mbalimbali na Wizara inayohusika na utumishi nayo inaendelea na zoezi kubwa linalohusisha masuala ya pensheni kwa ujumla wake.

Akizungumzia mafunzo kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina kabla ya kustaafu, alisema kuwa mafunzo yanaendelea kutolewa na yataboreshwa ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma hiyo.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Taska Restituta Mbogo, aliyetaka kufahamu lini Serikali itawaongezea pesheni wastaafu wanaolipwa shilingi 100,000 kwa mwezi na Hazina.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...