Na Elizaberth Msagula,Lindi

VIJANA waliohitmimu  mafunzo ya awali ya kijeshi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT)  wamehimizwa uzalendo,uaminifu na uadilifu katika kusimamia na kuijenga  nchi yao.

Yamehimizwa hayo na Brigedia Jenerali Charles Peter Feluzi wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa mujibu wa sheria oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Kikosi 843 Wilayani Nachingwea. 

Brigedia Jenerali Feluzi amewataka wahitimu hao kutumia mafunzo waliyoyapata katika kuijenga na kuilinda nchi  kwa kuzingatia kiapo chao huku akitaka wajiepushe na matumizi yasiyofaa katika mitandao ya kijamii na badala yake waitumie kujifunza na kwa manufaa bila kuvunja sheria na taratibu za nchi yao.

Luteni Kanali Nyagalu  Malecela ambaye ni mkuu wa kikosi cha 843 Nachingwea amesema vijana hao wakiwa kambini hapo kwa majuma 16  wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya awali ya kijeshi na kuwajenga vijana hao kuwa wakakamavu pamoja na wazalendo.

Awali akitoa salamu za Wilaya Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Haji Mbaruku Balozi aliwasihi wahitimu kuendelea kujiendeleza kimasomo.

"ni kwa kupitia Elimu kijana unaweza kuwa Meneja wa Benk, Mkuu wa kikosi, Mbunge , Waziri na Hata Rais hivyo niwasihi vijana kujiendeleza kimasomo ili mfikie malengo yenu" alisema Balozi.

Nao baadhi ya wahitimu  wakaeleza umuhimu wa mafunzo hayo sambamba na kuwasihi vijana wengine kujiunga na jeshi hilo.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...