Na Mwandishi Wetu

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limepokea taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kuhusu uwepo wa kimbunga “HIDAYA” katika Bahari ya Hindi mashariki mwa pwani ya nchi yetu.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC ilisema Kimbunga “HIDAYA” kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya pwani ya nchi yetu ambapo hadi kufika saa tisa usiku wa tarehe 03 Mei 2024 kilikuwa kimeimarika zaidina kufikia hadhi ya Kimbunga kamili kikiwa umbali wa takriban Kilomita 401 mashariki mwa pwani ya Mtwara.

Aidha taarifa hiyo ilisema tangu wakati huo,kimbunga HIDAYA kimeendelea kuimarika zaidi huku kasi ya upepo ikiongezeka hadi kufikia
Kilomita 130 kwa saa. 


TASAC inawataarifu wadau wote wa usafiri kwa njia ya maji kuwa mwenendo wa mifumo  ya hali ya hewa baharini bado unaonesha uwezekano mkubwa wa Kimbunga “HIDAYA”  kusalia katika hadhi ya Kimbunga kamili kwa saa 12 zijazo huku kikiimarika, na kendelea kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania.

Hata hivyo taarifa ilisema Kimbunga hikikinatarajiwa kuendelea kuwepo hadi tarehe 06 mwezi Mei 2024 na kupungua nguvu baada ya tarehe 6 Mei 2024.

Uwepo wa kimbunga hicho utasababisha ongezeko la mvua na upepo mkali utakaoambatana na mawimbi makubwa baharini yatakayosambaa katika eneo kubwa la mwambao wa bahari yetu.

Kwa msingi huo, TASAC inatoa wito kwa wadau wote wanaofanya shughuli za kiuchumi, wakiwemo wavuvi,kuchukua tahadhari na kujiepusha kufanya shughuli hizo baharini hadi hapo kimbunga kitakapopita katika mwambao wa bahari yetu. 

Kwa vyombo vinavyofanya shughuli za usafirishaji abiria,tunawaasa kuchukua tahadhari kubwa na kutumia taarifa
za hali ya hewa kabla ya kuanza safari.

Aidha TASAC imewaasa wananchi kwa ujumla kujiepusha na shughuli za starehe katika mwambao wa bahari hadi hapo kimbunga kitakapopita katika mwambao wa bahari yetu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...