Kadili siku zinavyozidi kusonga ndivyo teknolojia nayo inavyozidi kushika kasi na hapo ndipo Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo ilipoamua kuja kidijitali zaidi kwa kuzindua App ya kisasa kabisa ‘Super App’ ya Tigo Pesa ambayo itawarahisishia maisha watumiaji wa huduma za kampuni hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema App hiyo imekuja kufanya mapinduzi makubwa ya kuwarahisishia na kuwaboreshea maisha watumiaji wa mtandao huo kwa kutumia App hiyo mpya.

Angelica amesema kampuni hiyo ndiyo iliyoanza kuja na App ya kufanya miamala ya Tigo Pesa miaka kumi iliyopita lakini pamoja na mafanikio ya App hiyo wameonelea waje na App yenye ubora zaidi inayoendana na kipindi hiki ukilinganisha na ile ya miaka kumi iliyopita.

Ameendelea kusema baadhi ya vitu vilivyoboreshwa kwenye App hiyo ni pamoja na kuweza kufanya miamala kwa watu watatu kwa pamoja jambo ambalo awali halikuwepo, kununua vifurushi kirahisi zaidi, kufanya malipo mbalimbali na mengineyo.

App hiyo amesema ina kasi zaidi na ni rahisi kutumia ambapo inapatikana kwa watumiaji wote wa Smart Phone na Smart Kitochi.

Wateja wote watakaoipakuwa na kuanza kuitumia hiyo watapewa ofa ya GB 1 ya bure. Ama kweli Tigo yajayo yanafurahisha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...