Na. Mwandishi, Jeshi la Polisi – Arusha.
KATIBU  wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania TPF net Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Pili Mande amewataka Askari wa kike Mkoa wa Arusha kujiepusha na vitendo ambavyo ni kinyume na maadili ya Jeshi hilo.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akitoa mafunzo yaliyoandaliwa na mtandao huo kutoka makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwajengea uwezo Askari wa kike Jijini humo ambapo amewataka kutambua malengo mazuri ya kuanzishwa kwa mtandao huo.

Sambamba na hilo amebainisha kuwa Jeshi hilo halitasita kuchukua hatua kwa baadhi ya Askari wa kike ambao watabainika kutenda vitendo vya utovu wa nidhamu ikiwa ni pamoja na kuiga tamaduni mbaya za mataifa mengine,

Aidha amewataka kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo ili kuujua vyema mtandao huo juu ya malengo na madhumuni ya kuanzishwa kwake sambamba na kwenda kuboresha utendaji wa kazi na kutoa huduma bora kwa Wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kikosi cha Kuzuia Wizi wa Mifugo Nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Simon Pasua amesema askari wa kike wa Mkoa huo wamekuwa wakifanya kazi zote kwa kushirikiana na askari wakiume kitendo kilichopelekea Mkoa huo kuendelea kutoa huduma bora kwa wenyeji na wageni wanafika katika Mkoa huo.

Nae Mwenyekiti wa mtandao huo Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Debora Lukololo amesema kuwa watahakikisha wanayatumia mafunzo hayo vyema ili kuleta ufanisi wa utendaji wa majukumu ya askari wa kike Mkoa wa Arusha.

Sajenti Noela Pallagyo ambaye ni mshiriki wa Mafunzo hayo amebainisha kuwa mafunzo aliyoyapata yatamsaidia kuongeza ufanisi katika utoaji wa elimu dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia lakini pia kuisaidia Jamii kupaza sauti dhidi ya vitendo hivyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...