Mwanaisha Sendekwa akitoa elimu kuhusu Haki Miliki kwa wabunifu kutoka MUHAS wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika viwanja vya Popatlal,  jijini TangaAfisa Haki Miliki kutoka COSOTA, Mwanaisha Sendekwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wabunifu kutoka MUHAS baada ya kutoa elimu kwao juu ya haki miliki za kazi zao wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu  yanayofanyika katika viwanja vya Popatlal,  jijini Tanga

Na Mwandishi Wetu, Tanga
WABUNIFU kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili (MUHAS) wafaidika na mafunzo kuhusu umuhimu wa kulinda maslahi ya ubunifu wao na kutunza rejista za usajili wa kazi za kibunifu ili kupata uthibitisho wa umiliki ( copy right clearence) na kulinda kazi zao.

Akizungumza na wabunifu kutoka MUHAS, Afisa Haki Miliki kutoka COSOTA, Mwanaisha Sendekwa amesema uthibitisho wa umiliki ni haki ya kipekee ambayo inampatia mtunzi au mbunifu kipato kutokana na ubunifu wake na pia ni bidhaa ambayo huweza kuuzwa kwa mtu mwingine na kubadilisha umiliki.

” Ni muhimu kila mbunifu anapobuni ubunifu wa kazi yake anakuwa na hakimiliki na haki ya kiuchumi na haki za kimaadili ambazo zinasaidia usuluhishi wa migogoro ya uvunjifu wa haki miliki pale unapotokea” Alisema Mwanaisha.

Akizungumza leo Mei, 30, 2024, katika Mkutano uliandaliwa na Mratibu wa Ubunifu kutoka MUHAS, Dkt. Nelson Masota amesema mkutano huo lengo lake ni kuwakutanisha wabunifu kutoka MUHAS na mtaalamu kutoka Ofisi ya HakiMiliki (COSOTA) ili wapate elimu kuhusiana na masuala ya haki miliki.

Mkutano huu uliofanyika leo Mei 30 2024 kwenye maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea katika viwanja vya shule ya sekondari Popatlal , jijini Tanga uliandaliwa na Mratibu wa Ubunifu kutoka MUHAS, Dkt. Nelson Masota.

Amesema kuwa lengo kubwa la mkutano huo ni kuwakutanisha wabunifu kutoka MUHAS na mtaalamu wa COSOTA ili wapate elimu husika kuhusiana na masuala ya haki miliki. Na pia aliahidi kuwaalika wataalamu hao kutoka COSOTA kuja MUHAS ili watoe elimu hiyo kwa kina zaidi kwa wabunifu wa MUHAS.

Pia amesema utawafungua macho wabunifu hao wanaokwenda kuzitambulisha kazi zao sokoni kukabiliana na changamoto hatimiliki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...