Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) inaendelea na kazi ya utoaji mafunzo kwa Walimu Wakuu wa shule za msingi za Serikali na zisizo za Serikali nchini kwa lengo la kuwajengea uelewa wa namna bora ya kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa Mtaala wa Elimu ya Awali na Msingi wa Mwaka 2023.

Akizungumzia kuhusu mafunzo Mkurugenzi Mkuu wa TET , Dkt. Aneth Komba amesema kuwa mafunzo hayo yatafanyika Kwa walimu Wakuu wote katika Halmashauri 184 kuanzia leo tarehe 5/5/2024 hadi 12/6/2024 kwa awamu tofauti ambapo katika awamu ya kwanza, mafunzo yatafanyika katika Halmshauri za Mkoa wa Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kagera Kigoma, Geita na Tabora.

“Tunaendelea na mafunzo na awamu hii ni ya walimu wakuu wote nchi nzima ambapo tufanafaya mafunzo kwa awamu tofauti tofauti”amesema Dkt.Komba.

Aidha, Dkt. Komba ameeleza kuwa mafunzo ni ya muhimu kwakuwa walimu Wakuu wataweza kusimamia na kufuatilia utekelezaji wake na kuweza kutoa msaada (Mentorship and Support) kwa walimu wengine masomo pale inapohitajika.

Wawezeshaji na waratibu wa mafunzo hayo ni kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, OR-TAMISEMI na TET,huku akiishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongzwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwezesha mafunzo hayo kufanyika kwa walimu wote nchini.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...