Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Bw. Charles Asiedu alipowasili katika kikao kilichoangazia ushirikiano kati ya Serikali na benki hiyo, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Bw. Charles Asiedu, kuhusu ushirikiano kati ya Serikali na benki hiyo, alipomtembelea katika ofisi za Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank Tanzania, Bw. Charles Asiedu, akimuelezea Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), mafanikio ya benki hiyo wakati alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza na ujumbe wa Ecobank Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Bw. Charles Asiedu, jijini Dodoma.
Kamishna Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, akifafanua jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), na ujumbe kutoka Ecobank Tanzania, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiuongoza ujumbe wa Wizara hiyo katika picha ya pamoja na ujumbe wa Ecobank Tanzania ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Bw. Charles Asiedu, baada ya kikao kilichoangazia ushirikiano kati ya Serikali na benki hiyo, jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...