Anthony Mgaya (50) aliyekuwa Katekista wa Kigango cha Moronga kata ya Kipengere wilayani Wanging'ombe amefariki dunia akidaiwa kunywa sumu kutokana na msongo wa mawazo wa muda mrefu uliotokana na kifo cha mfadhili wake ambaye alikuwa wilayani humo aliyefariki takribani miaka miwili iliyopita.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Mahamoud Banga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

"Majira ya saa nane mchana alikutwa nyumbani kwake na mkewe anaitwa Huruma Mbilinyi akiwa ananukia harufu ya sumu aina ya daiso ambayo ilikuwa store alivyokwenda store kukagua mabaki ya ile sumu kwa ajili ya kuulia wadudu hakuikuta kwa hiyo akaamini huyu bwana ameinywa ndio wakamchukua na kumpeleka hospitalini"ameongeza kamanda Banga

Banga ametaja sababu ya kifo hicho "kwa hyo sababu kubwa ni msongo wa mawazo ambapo alikuwa akifadhiliwa na mzungu ambaye alifariki muda si mrefu sana na toka alipofariki Mzungu huyu bwana akaanza kupata shida ya msongo wa mawazo jambo ambalo limepelekea kujitoa uhai wake"

Katika mazishi ya katekista Anthony Mgaya mwenyekiti wa kijiji cha Moronga Romanus Mgaya ametoa wito kwa wananchi kushirikisha jamii juu ya changamoto zinazowakabili hususani mawazo ili waweze kukabiliana nazo kuliko kuwa kimya na kuelemewa nazo hali inayopelekea vifo na kuacha familia ikiwa tegemezi.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...